Swahili
Home » Rwanda kupiga marufuku kumkamata Mnyarwanda nchini Uganda
HABARI MPYA KIMATAIFA

Rwanda kupiga marufuku kumkamata Mnyarwanda nchini Uganda

Mnyarwanda,Emmanuel Cyemayire

Kwa mujibu wa taarifa Chimpreports,wizara ya mambo ya nje ya Rwanda inatarajia kupiga marufuku wiki hii kitendo cha kumkamata  Mnyarwanda Emmanuel Cyemayire ambaye alikamatwa wiki iliyopita aipokuwa mjini Mbarara.

Emmanuel Cyemayire ambaye ni mwenyeji wa duka mjini Mbarara, alitoweka baada ya watu wenye silaha tarehe 4 Januari 2018 saa mbili usiku kumuweka garini na kuelekea mahali ambapo hapakujulikana kwa mashahidi hadi kwa sasa.

Bi Cyemayire, Yvonne Mukakalisa ametangazia Chimpreports kwa kuhakikisha kwamba mumewe alitekwa nyara na watu wenye silaha waliokuwa wakiendesha gari la aina ya lori(double cabin truck).

Kuna taarifa kwamba Rwanda inajianda kuuliza Uganda kuhusu suala hili wakati ambapo Cyemayire hayupo kwenye kituo cha polisi.

Hili ni baada ya Uganda kueleza kwamba Wanyarwanda wanaokamatwa nchini Uganda ni wale ambao wanahusiana na vitendo vya upelelezi na ugaidi nchini humo.

Haya yanatokea baada ya ziara yake waziri wa mambo ya nje wa Uganda,Sam Kutesa nchini Rwanda ili kujadiliana na Rais Kagame kuhusu namna ya kutoa suluhisho kwa changamoto za ushirikiano zilizozuka miezi michache iliyopita.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com