kwamamaza 7

Rwanda kuomba nchi nyingine msaada wa kupiga marufuku uamuzi wa jaji Meron

0

Makamu Waziri wa mambo ya nje, Olivier Nduhungirehe ametangaza Rwanda inatarajia kutaka nchi nyingine msaada wa kupiga marufuku uamuzi wa kuachia huru mapema wafungwa wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi 1994

Huyu kiongozi ameelezea watangazaji  kuwa Rwanda ingali katika mazungumzo na nchi nyingine kuhusu marufuku uamuzi ya jaji Theodor Meron,88, anayetaka mamlaka nyingine.

“ Hatuzungmzi na Urusi tu kuhusu hili suala, ni nchi zote kwa kutusaidia kulaani haya. Anachofanya Meron ni matusi kwa walionusurika na kutotii sheria” Nduhungirehe alisema

“Tutaendelea kuzungumza na nchi zote ili haya mambo ya Theodor Meron yasiendelee” aliongeza

Nduhungirehe amesisitiza Rwanda ina wasiwasi ya namna ambavyo wanaoachiwa huru ni wale ambao hawakukubali kuwa yalitokea mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994

Pia Rwanda iliandikia Urusi kuhusu hili suala kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa(YUNA).

Jaji Meron aliwaachia huru mapema wafungwa wa  mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi 1994 wakiwemo Nahimana Ferdinand na Padiri Rukundo Emmanuel waliokuwa nchini Mali.

Wengine ni Zigiranyirazo Protais, Mugenzi Justin, Mugiraneza Prosper, Gen. Ndindiriyimana Augustin na Major Nzuwonemeye François Xavier.

Fred Masengesho rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.