kwamamaza 7

Rwanda kukaribisha wahamiaji maelfu 30 wanaoteswa kiutumwa nchini Libya

0

 

Serikali ya Rwanda imeweka wazi nia ya kuwakaribisha wahamiaji maelfu 30 wanaoteswa kiutumwa nchini Libya.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda,Louise Mushikiwabo ameleza kuwa kuna mazungumzo ili kutafuta namna ya kusaidia wahamiaji waliotekwa nyara nchini Libya.

Pia ameongeza kwamba uamuzi umeisha tolewa na kuwa mambo husika na  idadi yao namna ya usafishaji yangali katika mahojiano.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Waziri Mushikiwabo amesema”Rwanda inatarajia kuwakaribisha wakimbizi karibu elfu 30”.

Haya ni baada ya hotuba ya Mkurugenzi wa Tume ya Umoja wa Afrika,Moussa Faki Mahamat akihamasisha washirika wa Umoja wa Afrika kuungana mkono kwa kutatua suala la wakimbizi wanaouzwa kwa mnada nchini Libya.

Taarifa za The East African zinasema kuwa Waziri Mushikwabo alitangazia  AFP kuwa Rwanda ilisikitishwa na maovu yanayotendewa wahamiaji waliogeuzwa watumwa nchini Libya.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Rwanda imeamua kufanya jambo hili baada ya picha zilizochukuliwa na CNN kuenea zikionyesha kijana mhamiaji akiuzwa kwa mnada $400.

Kulingana na takwimu za shilika la kimataifa la wahamiaji,juu ya wahamiaji 8,800 wameisha rudi nyumbani kwao mwaka huu,jambo ambalo ni dalili ya utumwa wanaofanyiwa nchini Libya wakitaka kuelekea Ulaya.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.