Swahili
Home » Rwanda kuanzisha taasisi ya kupambana na wadukuzi wa mtandao
USALAMA

Rwanda kuanzisha taasisi ya kupambana na wadukuzi wa mtandao

Ikiwa kuna ongezeko kubwa la kesi za udukuzi wa mitandao ambazo zilijitokeza kwenye siku za hivi karibuni serikali ya Rwanda inapanga kuanzisha taasisi ya kupambana na wadukuzi wa mitandao.

Muhizi Innocent ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Nchi lenye Mamlaka ya Mawasiliano(RISA), amesema kwamba kuanzishwa kwa taasisi hiyi kunalenga kuimarisha kupambana na udukuzi wa mtandao. Mkurugenzi huyu ameonya kwamba ingawa kesi hizi hazijakuwa nyingi nchini Rwanda hakuna sababu yoyote ya kulichukulia kiholela.

Ripoti iliyotangazwa na Shirika la Kimataifa la Mawasiliano imeiweka Rwanda kwenye nafasi ya pili ikifuata Mauritias barani Afrika.

Takwimu za jinsi nchi zinavyopambana na udukuzi wa mtandao zinaonyesha kwamba  Rwanda vilevile inashika nafasi ya pili barani afrika.

Mambo yanayotiwa maanani ni taratibu za nchi za kupambana na udukuzi kwenye ngazi ya sheria, tekniki, mifumo ya uongozi, kujijengea uwezo na ushurikiano wa kimataifa.

“kwa kuwa usalama wa mitandao una maana kubwa, Serikali inapanga kuianzisha taasisi huru ambayo itakuwa na majukumu ya kupambana na udukuzi wa kimtandao” asema Muhizi

Mkurugenzi huu aliendelea kusema kwamba mpaka sasa Rwanda ina uwezo wa kugundua na kusimamisha uvamizi wa mitandao.

“Tunahitaji kiwango maalum cha kugundua na kujibu uvamizi fulani wa mitandao. Naweza kusema kwamba tuko salama kwelikweli, siyo!” asema Muhizi.

Shirika hili la nchi la mawasiliano limepewa hivi awali majukumu ya kujadili na habari, mawasiliano na teknolojia na kukuza ustadi wa ICT ambazo zimekuwa zikishikiliwa na RDB.

Kwa kukabidhi RISA na majumu hayo Bodi hii ya Maendeleo ya Nchi itasalia na majukumu ya kukuza uwekezaji.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com