kwamamaza 7

Rwanda: Klezia Katoliki yapinga  matumizi ya uzazi wa mpango wa kisasa

0

Klezia Katoliki nchini Rwanda imekanusha matumizi ya mbinu za uazazi wa mpango wa kisasa katika hospitali na hazanati zake nchi nzima.

Kufuatia hatua hii, klezia imetoa amri viongozi wa hospitali hazanati zake wairudishie serikali pesa zake ilizotoa kwa mradi huu kabla ya tarehe 30 Juni mwaka huu.

Pia imekataa mpango wowote husika na mradi huu. Klezia ilitangaza mwaka 2016 kwamba imekomesha matumizi ya uzazi wa mpango usio wa kimaumbile.

Hata hivyo, Waziri wa Afya nchini Rwanda, Dk. Diane Gashumba amesema uamuzi huu ni kipingamizi kwa serikali.

“ Uamuzi huo ulinifanya niogope kama waziri wa afya.” Amesema

“ Wakigoma kupoke msaada wa serikali, hatuatweza kuwapima wananchi virusi vya ukimwi kwa wanawake, wajawazito, kupamabana na utapia mlo n.k.” Waziri  Gashumba ameongeza.

Askofu Filipo Rukamba, Msemaji wa Baraza la Maskofu nchini Rwanda ameambia vyombo vya habari nchini kwamba jambo hili si mpya.

Amesema kwa kawaida, Klezia Katoliki haikubali matumizi ya uzazi wa mpango usio wa kimaumbile.

Ameitaka serikali itumie namna nyingine kutoa suluhisho kwa suala hilo.

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.