kwamamaza 7

Rwanda: Kiongozi wa wanagamgambo atiwa hadharani

0

Msemaji wa wanamgambo, Callixte Nsabimana maarufu kama Sankara ameonyeshwa wananchi leo baada ya kukamatwa mwezi uliopita.

Sankara aligonga vichwa vya habari juu ya kutangaza kwamba amekaba sehemu ya mwitu wa Nyungwe, Kusini Magharibi mwa Rwanda.

Akizungukwa na polisi kila upande, ameonaka mzima kama kigongo akiangua kicheko mala chache.

Rwanda imeeleza kuwa Sankara alikamatwa tarehe 13 bila kueleza alikamatiwa wapi. Hata hivyo, kuna ripoti kuwa alikamatwa huko Visiwani Mayotte halafu akapelekwa nchini Rwanda.

Sankara hakusema lolote, ila mwanasheria wake, Moise Nkundabarashe amewambia watangazaji kuwa mashtaka yatajulikana siku zijazo.

“ Baadhi ya wanasheria walilaani kazi hii lakini ni haki yao. Alinicahagua yeye nimuwakilishe kisheria.

Anashtakiwa mashtaka yakiwemo vitendo vya kigaidi, kuunda jeshi kinyume na sheria n.k.

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.