Swahili
Home » Rwanda: Kiongozi awatukana wapinzani” Ni jamii kubwa ya wajinga”
HABARI MPYA

Rwanda: Kiongozi awatukana wapinzani” Ni jamii kubwa ya wajinga”

Kiongozi wa mambo ya ‘Itorero’ nchini Rwanda,  Edouard Bamporiki ametangaza Rwanda haina adui  na kuwa wapinzani ni jamii kubwa ya wajinga

Bamporiki alifunguka haya tarehe sita mwezi huu alipokuwa mjini Coventry,nchini Uingereza.

Huyu alieleza Rwanda imetekeleza mengi kutokana na chama tawala RPF na kuwa hakuna adui wa Rwanda kwa kuwa hadui ambaye hakushambulii  huwa anajidanganya.

“ Rwanda haina adui, ina watu waliopotea njiani. Ni jamii kubwa ya watu ambao ni wajinga” Bamporiki alisema

“ Huwezi kusema kwamba una adui asiyekushambulia na hamshindani. Unapomuambia kuwa yeye ni adui inampa nguvu. Muambie alipoteza njia,arudi nchini” aliongeza

Pia Bamporiki amewalaumu marais wa Rwanda hasa Meja Jen. Juvenal Habyarimana kwa kusema hawakutayarisha njia za kuongoza nchi kama walivyofanya wafalme.

Kwa mala nyingi wapinzani wanasikika wakimunyoshea kidole Bamporiki kwamba anasema maneno matamu kwa serikali.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com