kwamamaza 7

Rwanda: Kijana auawa kwa kumficha mtu aliyetega kazi za kijamii

0

Kijana Hussein Mbabariye,19, wilayani Nyanza  Kusini mwa Rwanda leo jumamosi ameuawa na walinzi wa usalama maarufu kama ‘Inkeragutabara’ juu ya  kumficha mkazi aliyetega kazi za kijamii kwa jina la ‘Umuganda’.

Katibu mtendaji wa tarafa ya Busasamana amehakikisha taarifa hizi kwa vyombo vya habari kwa kusema wanausalama maarufu  wamempiga na kumuua huyu kijana ambaye hakufanya kosa lolote isipokuwa kugoma kuwaonyesha anapokijificha mtegaji wa kazi za kijamii.

Msemaji wa Ofisi Kuu ya Upelelezi, Mbabazi Modeste ametangazia Ukwezi kwamba aliyeuawa alikuwa hana kosa lolote.

“ Huyu kijana hakuwa na kosa lolote,wanausalama wamemuuliza mwenzake aliyekimbia na akakataa kuwaeleza na wakampiga kisha akafariki”

Kwa sasa, mmoja mwa Inkeragutabara amekamatwa ili kufuatilia sheria.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com
 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.