Swahili
Home » Rwanda imeomba Tanzania waalimu wa lugha ya Kiswahili
HABARI MPYA

Rwanda imeomba Tanzania waalimu wa lugha ya Kiswahili

Taarifa kutoka Tanzania husema kwamba wizara ya Elimu kamufikishia rais Magufuli barua kutoka kwa rais Kagame akiomba waalimu wa kufundisha lugha ya Kiswahili Rwanda.

Kupitia mtandao wa East African Radio, husema kuwa waziri wa elimu, Dr Papias Musafiri kuwa ndiye alimufikishia rais Magufuli barua hio.

Husemekana kuwa rais Magufuli alifurahia kuwa Rwanda waliamua kufundisha lugha ya Kiswahili shuleni na akasema yupo tayari kupana waalimu wa Kiswahili.

Katibu wa serikali ya Rwanda anayehusika na shule la msingi na sekondari, Isaac Munyakazi, alihakikisha kuwa waziri Musafiri yupo Tanzania. Alisema kuwa kuna yale waziri Musafiri aliyo yaongea na upande wa Tanzania ila hana mengi ya kutangaza, aliambia mwanahabari kusubiri hadi waziri arejee kama vile husema izubarirashe.

Siku nenda Rwanda iliwapa kazi watu kutoka mataifa wa kufundisha kingereza wakati Rwanda ilikubaliwa katika nchi ambazo hutumia kingereza (Common Wealth).

Kiswahili hufundishwa katika mashule machache, zamani walio fuata masomo ya lugha walikuwa wakijifunza hata Kiswahili ila kwa sasa kuna wale ambao hawajifunzi tena Kiswahili kama EFK.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Rwanda humaliza miaka 10 wakiwa katika jamii ya Afrika ya Mashariki na Kiswahili ni Lugha ambayo hutumia sana na nchi hizo.

Baada ya serikali na bunge kuamua kuongeza Kiswahili kama lugha rasmi Rwanda, wanahabari wanaosema Kiswahili waliunda kundi lijulikanalo kwa jina la WAKIRWA wakiwa na lengo la kuendeleza lugha ya Kiswahili.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Leki/bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com