kwamamaza 7

Rwanda: Idadi ya watu wanaoaga dunia kwa Malaria yapunguzwa

0

Wizara ya afya imetangaza kuwa idadi ya watu wanaokufa kwa malariya imepunguzwa kwa kuwa watu 400 wameaga dunia mwaka 2017 kinyume na 715 mnamo mwaka 2016

Mzazi na mtoto wake wakilala ndani ya chandarua ili kujilinda malaria

Akiongea na Radiyo Rwanda,kiongozi wa mkondo wa huduma za msingi za kutibu malaria kwenye bodi kuu ya afya (RBC),Aline Uwimana ameweka wazi kuwa idadi ya watu wanaokufa kwa malariya ilianza kupunguzwa mwaka 2014.Amesema kuwa watu 499 walikufa mwaka huu na 424 mnamo mwaka 2015 kwa ajili ya mipango mbali mbali iliyoanzishwa na serikali,amesema”Hivi ni vipimo vinavyoonyesha kuwa kuna mafanikio mazuri”.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Uwimana amendelea kusema kwamba ili kupamabana na malariya serikali ilisuluhisha kuleta madawa  na vifaa kama TDR (Teste de Depistage Rapide) karibu na wakazi hadi huko vijijini na kuwa  watu ambao ni wa daraja la kwanza na la pili wanatibiwa kwa bure,daraja la tatu na nne wakiwa na bima ya afya hulipa 200 ikiwa hawana hulipa 500.

Kiongozi huu amehamasisha wakazi kwenda hospitali mapema wakiona ishara za ugonjwa wa maraliya kama vile  kutapika,joto,kutokwa jasho na mengine na kusisitiza  kuwa serikali itaendelea kuwasaidia kupitia mipango yake kama vile kunyunyisia madawa ya kuua mbu wa kike(anophele) na kutoa chandarua.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.