Swahili
Home » Rwanda haikufurahia kuachiliwa huru kwa wafungwa wa mauaji ya kimbari Mali
SHERIA

Rwanda haikufurahia kuachiliwa huru kwa wafungwa wa mauaji ya kimbari Mali

Mahakama ya kimataifa kwa ajili ya Rwanda imewaachia huru wafungwa wawili wa mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi kabla ya kumaliza vifungo vyao. Ferdinand Nahimana na Padri Emmauel Rukundo walikuwa wamehukumiwa kufungwa jela miaka 30 na 23 mtawalia kwa makosa ya kutekeleza mauaji ya kimbari.

Wote walikuwa katika jela ya Koulikoro nchini Mali na mahakama imesema wamekamilisha theluthi mbili ya vifungo vyao na wamekuwa na mwenendo mzuri gerezani.

Uamuzi huu haujapokelewa vyema na serikali ya Rwanda.Msemaji wa ofisi ya mashtaka ya Rwanda Faustin Nkusi ameambia BBC kwamba hawa watu walikuwa miongoni mwa viongozi waliopanga na kutekeleza mauaji ya kimbari.

[ad id=”72″]

“Kweli ni utaratibu wa kisheria lakini haujatufurahisha kwa sababu kwanza hukumu waliyokuwa wamepewa ni ndogo ukilinganisha na mchango wao katika mauaji hayo, sasa leo unasema waachiwe huru eti walikuwa na mwendendo mzuri?”

Sababu zilizotolewa na jaji Theodor Meron ambaye pia ni mkuu wa chombo kilichochukua mikoba ya mahakama ya kimataifa kwa ajili ya Rwanda, ni kwamba japo watu hao walipatikana na hatia ya makosa makubwa waliweza kuonyesha mwendendo mzuri wakiwa gerezani na kwamba wamekamilisha theluthi mbili ya vifungo vyao.

[ad id=”72″]

Watu 10 tayari wamekwishaachiliwa huru na mahakama hiyo kabla ya kumaliza vifungo vyao miongoni mwa wafungwa 61 waliohukumiwa na mahakama hiyo kwa hatia ya mauaji ya kimbari.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com