Dini ya kikatoliki nchini Rwanda iliwaombea msamaha waamini wake walioshiriki katika mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi yalipatikana mnamo mwaka wa 1994 yaliyosababisha vifo zaidi ya milioni  ya watutsi nchini Rwanda.

Msamaha huo uliombwa katika barua iliyotiwa saini na maaskofu tisa kwa niaba ya dini ya Kikatoliki nchini Rwanda na kusomewa mbele ya wakristo nchini kote siku ya jumapili iliyopita.

Barua inasema kwamba ingawa Dini ya Kikatoliki haijawahi kushiriki mauaji ya kimbari kama taasisi kwa ujumla , lakini kuna wakristo wake waliotenda jinai la mauaji ya kimbari.

[ad id=”72″]

“ingawaje hakuna mtu aliyetumwa na Katoliki kwa kufanya mauaji, sisi maaskofu tunaomba msamaha kwa baadhi ya wakristo , wakuu wa dini, watu waliojitolea kwa kumtumikia Mungu lakini wakakosa njia ya ujumbe waliopewa na mungu na wakatenda mauaji ya kimbari.”

“sisi maaskofu, tunaomba msamaha kutokana na uhalifu mbalimbali uliofanywa na wakristo na wakuu wa dini ya kikatoliki, tunasikitishwa na wenzetu waliopuuza ujumbe wa mungu katika amri zake ubatizo kisha wakaua jirani na marafiki zao.’’

Askofu Philippe Rukamba wa dayasisi ya Butare ambaye ni msemaji wa dini ya katoliki nchini Rwanda alisema kwamba wao waliandika tamko hili kwa kuonyesha kuwa mauaji ya kimbari ni mpango uliopangwa na serikali iliyokuwa madarakani, Dini ya Kikatoliki hakukuwa uhusiano na mpango huo.

[ad id=”72”]

Mnamo miaka iliopita baada ya tukio la mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi yalipatikana nchini Rwanda, kanisa la mtaa lilipinga msisitizo wa serikali na shirika za walionusulika wa kuomba msamaha juu ya ushiriki katika mauaji ya kimbari; ikisema kwamba walioshirika hawakufanya kwa niaba ya dini na kanisa.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Bwiza.com

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.