kwamamaza 7

Rwanda: Asilimia 60 za wakimbizi asili ya DR Congo katika kambi ya Kiziba wajiandikisha kurudi kwao

0

Shilika la kuhudhumia wakimbizi (UNHCR) nchini Rwanda limetangaza asilimia sitini za wakimbizi asili ya DR Congo katika kambi ya Kiziba, magharibi mwa Rwanda wamejiandikisha kurudi nyumbani kwao.

UNHCR imeeleza maafisa wake wataendelea kuwasajili wakimbizi wenye nia ya kurudi kwao.

Kupitia mazungumzo na BBC, hili shilika limeeleza tukio hili litaendelea hadi mwezi  Ogasti 2018.

Hawa wakimbizi walionyesha hamu ya kurudi nchini kwao baada ya wenzao 11 kufariki wakati wa maandamano mwezi Februari.

Hivi Karibuni, Serikali iliwafunga wakimbizi 44 kwa kuwashtaki kudharau sheria za ndani.

Kambi ya Kiziba,magharibi mwa nchi,inawahudhumia wakimbizi asili ya DR Congo 17,000 tangu mwaka 1996.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.