kwamamaza 7

Rwamagana:Wakazi wanung’unika juu ya huduma ovyo za bima ya afya

0

Wakazi wa tarafa ya Kigabiro,wilaya ya Rwamagana wameweka wazi kuwa hawafurahi juu ya huduma mbaya za bima ya afya wanazopatiwa na viongozi wa mitaani.

Hawa wametangaza kuwa wametafuta miaka nenda rudi kadi za bima ya afya na kukosa kinyume na kuwa walilipa fedha zao.

Mmoja wa hawa ambaye ni mkazi wa kijiji cha Cyanya ametangazia Bwiza.com kuwa amemaliza miezi sita bila kadi yake ya bima ya afya hata kama alilipa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Afisa kwa wajibu wa mambo ya kijamii wa tarafa ya Kigabiro,Emmanuel Mikebanyi ameleza kuwa kuna swala la uhaba wa intaneti kwenye ofisi za vijiji na kuwa wanatarajia kutoa intaneti kwa kutatua swala hili kwa kuwa ndilo chanzo cha huduma mbaya za utoaji wa bima ya afya inayojulikana kama ’Mutuelle’.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pamoja na haya wilaya ya Rwamagana ina mkataba wa utendaji kwa bima ya afya kuwa ulitimizwa kwa kiwango 84.3% mwaka uliopita.  

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.