kwamamaza 7

Rwamagana: Raia wanahitaji serikali kuwapokonya wafugaji mashamba ili waweze kuyatumia

1

Raia wa wilaya ya Rwamagana, sehemu za Kigabiro, Muhazi,Fumbwe na Gahengeri wanadai kwamba ni tatizo kwao kwa kuwa mashamba yenye majimaji yalinyukuliwa na wafugaji wanaopafugia mifugo yao ,na wanaomba warudishiwe mashamba hayo ili waweze kuyazalisha mali.

Mashamba haya yalikuwa ndio asili ya mazao yao,kwa kuwa walikuwa wakipanda mimea ili ije ikawasaidia nyakati za ukavu. Raia hawa wanasema kwamba kuna mashamba yaliyozalishwa mali na kuwashtumu wanamali kuyanyakua mshamba yote ili waweze kupafugia mifugo yao

‟ Matajiri wengi unawakuta ni wafugaji, wanaponunua shamba kavu lililo karibu na lenye majimaji wanalitumia kama mahali pa kufugia na tukadhani wamelinunua kwa ujumla wakati inasemekana mashamba ya majimaji ni milki ya serikali, walioyazungusha ua mashamba wangezipokonywa ingetusaidia kwa kuwa tungelima katika misimu ya jua kali, unakuta mahali ambapo pangelimwa na watu wapatao 50 panahifidhiwa ng’ombe wa tajiri fulaniˮ raia mmoja akasema

Raia mwingine ambaye hakupenda kutajwa jina alithibitisha kwamba kulikuwa na mahali mojawapo kulipogawa mashamba yenye majimaji lakini wanaomiliki vipande pana hawakugusiwa ili wapokonywe mashamba hayo.

“Kwa mfano hivi katika shamba lililokuwa la Padre Dominiko liligawa kwa raia ili waweze kulilima lakini baado hakuwa yeye pekee ambaye ni mmilki wa hifadhi ya mifugo iliyounganishwa na shamba lenye majimaji. Kwa mfano wa Modeste anamiliki kipande kipana cha shamba lenye majimaji mbalo limekuwa ndio asili ya ruzuku lakini sasa hakuna yeyote angethubutu kupalima kwa kuwa tulikwisha jua ni mali ya Modeste na alipazungusha ua akaambatisha shamba hilo alilokuwa nalo hapo Cyahafi na lile la Rutonde, shamba la majimaji lililokuwa mpaka wa Rutonde ,Cyahafi na sehemu zingine tulikwisha fahamu ni mali ya Modeste ”. alisema raia

[xyz-ihs snippet=”google”]

Aliendelea kusema “Ukichukua mfano wa shamba lenye majimaji la Rupfumfuri katika Sibagire napo kuna mwanaume ambaye alipanyakua na kupatumia kadhiri anavyotaka na hakuna raia ambaye angethubutu kwenda kupalima”.

Viongozi wa wilaya walikiri kwamba kuna mashamba waliyopewa raia ili yaweze kutumiwa ipasavyo.

Mudaheranwa Regis, makamu-meya anayejadili maswala ya uchumi alikiri kwamba hakuna mtu yeyote aliepokonywa ardhi kwa ajili ya mwingine bali wamekopwa ardhi hiyo kwa kuwa imekuwa ikitumiwa kiholela.

“ Kuna shamba lililoko sehemu za Nyagasenyi ambalo lilipewa raia kwa ajili ya matuzi yenye kuzaa faida, lakini pia kulikuwa na lengo la maandalizi ya msimu wa kilimo,baadhi ya mashamba hayo anaweza pia kulimwa hata nyakati za jua kali“ aliendelea kusema.

Alisema zaidi kuwa mashamba ambayo haitumiwi ipasavyo, wamilki wake wanahimizwa kuyatumia kulingana na lengo lake la sivyo wanyanganywe kwa mujibu wa sheria

Alisema “ kama mmilki wa ardhi fulani yaitumii ipasavyo ,anapewa maonyo akifeli ananyanganywa na kupewa wengine ambao wataweza kuitumia ipasavyo, kuhusu uwezekano wa wamilki haramu hilo ni swala ambalo litabudi kutatuliwa na ngazi husika wakiwemo one stop center.

Ingawa raia wanakiri kwamba kuna mashamba yenye majimaji yaliyoporwa na wafugaji, mashamba kama hayo anahesabiwa kama milki ya serikali kama anavyotibisha pia Nyirarukundo Ignatienne, mbunge katika idara ya kilimo ya Bungeni

Katika mazungumzo na Bwiza.com kupitia simu, alhamisi ya tarehe 25 Mei 2017 alisema “ ardhi yote ni milki ya serikali mwenye kudai kumilki anapaswa kuitumia ipasavyo, hususani mashamba hayo hayo hutumiwa kwa kulima bali angewekupo yeyote anaeitumia ardhi hiyo kiholela, madaraka ya wilaya ikishirikiana na one stop center watalazimu kujadili swala hilo”.

Anaendelea kusema kuwa hilo si swala gumu kwa kuwa kuna sheria zinazobainisha ni ipi ardhi ya serikali na isilo yake.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Richard Wa Billy/bwiza.com

1 Comment
  1. MM says

    Maoni yangu ni kwamba kamwe wafugaji na wakulima hawawezi kuelewana kwani chuki baina watu hao si ya leo pekee baali tu tangu zamani lkwa enzi za zamani !

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.