Swahili
Home » Rutsiro:Waschana 400 waliozaa bila ndoa wanaishi katika hali mbaya
HABARI

Rutsiro:Waschana 400 waliozaa bila ndoa wanaishi katika hali mbaya

Waschana 400 kutoka vijiji vitatu vya tarafa ya Kivumu, wilaya ya Rutsiro wanaishi katika hali mbaya baada ya kuzaa watoto bila ya kufunga ndoa na kuwa miongoni mwao wameisha ambukizwa virusi vya ukimwi na hata hawana mahitaji ya msingi jambo linalowasababisha kujihusisha na ukahaba.

Waschana hawa ambao wanaungana mkono katika ushirika wa’Twigarurire icyizere’ iliyoundwa na mwenyeji wa huko, wengi hawakumaliza masomo yao wanatumia kwa kukodi vyerahani vitatu tu kwa kufuma nguo za kienyeji na kadhalika.

Hawa wanaonyesha matatizo mbalimbali yakiwemo ufukara ambao unawasababisha hata kufanya mapenzi bila kutumia kondomu.Wanao virusi vya ukimwi hawana woga wowote wa kuambuiza kwa wingi wanaume wanaowapatia fedha kulingana na tangazo kutoka City Radio.Mmoja wao amesema”Nilifanya mapenzi na mume  na kunipachika mimba,sasamimi na mwanangu tunaishi katika hali ya umaskini…”.

Mwenza ke amabaye jina lake halikutajwa ameeleza sababu malumu  yao kujihususha na mambo ya ukahaba akisema kuwa ni umaskini na kukosa chakula cha kujitunza katika maisha yao ya kila siku,na kusema”Ukahaba ni kwa ajili ya hali mbaya ya maisha yetu,kwa mfano mwanangu hawezi kukosa chakula cha mchana au cha jioni ambacho hakitoshi,nikimkuta tajiri humaliza mambo na mwanangu akapata chakula”.

Wengi wao hawaogopi kamwe virusi vya ukimwi kutokana na hali mbaya  ya maisha waliyowahi kuishi zamani kama vile kukosa malezi ya familia zao kwa umri mdogo na kukodi wenyewe katika vijiji tofauti kama Kavumu.Mmoja ameeleza”Waweza kuogopa virusi vya ukimwi ukiwa na shibe lakini ukiwa na njaa hukumbuki”

Mwingine amesema kwamba ana virusi vya ukimwi na anamiliki watoto watatu wenye baba tofauti na kuwa mwanamume akimpatia 1000 anakubali kufanya mapenzi na ye bila kondomu.Ameongeza kuwa yeye anatoa maonyo  kwa mwenzake kabla ya kuanza vuguvugu la kitanda kwamba ana virusi vya ukimwi, ili ajikinge mengine akatoa suluhisho lake la kujikinga ama kutojikinga,kwa kujikinga hupatiwa 400 na kinyume 1000.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Hawa Waschana wanaomba serikali kuwasaidia ili waache ufukara nao wapige hatua ya maendeleo.Kwa upande wa serikali wanasema kuwa haya yote ni matokeo ya wazazi kutofanya vilivyo wajibu wao.Katibu mtendaji wa tarafa ya Ruvumu,Bisangabagabo Sylivestre amesema kwamba uja uzito usio na mpango ni sababu ya malezi duni ya wazazi.Sylivestre amesema”Ni malezi duni ya wazazi,kusoma ni bure.Tunahamasisha wazazi kuendelea kulea watoto vilivyo na kutokata tamaa”.

Kiongozi huu amaeongeza kuwa anaomba waschana kujirinda virusi vya ukimwi na kuwa serikali iko tayari kuwasaidia kupitia mikakati mbalimbali kama vile kuahukumu wanaume wanaozaa  watoto badaye wakagoma kutoa mahitaji ya msingi.Akisema”Tatizo kubwa ni kuwa watoto hawa baada yakuzaa wanahisi aibu na kuamua kutorudi kwao kwa kuwa wanadhani kuwa wameisha geuka watu wazima, lakini hili si tatizo kubwa sana”.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com