kwamamaza 7

Rutchuru: Wapiganaji wengine wameanza kuwasili kundi la M23

0

Uongozi wa uraia katika wilaya ya Rutchuru, jamhuri ya kidemokrasia ya Congo husema ya kuwa wapiganaji walio kuwa kati jeshi la nchi wameanza kuwasili wapiganaji wa M23 na makundi mengine kwa sababu walitoshwa katika jeshi la taifa bila vifaa vya kuwasaidia kuyaanza maisha mapya.

Mmoja wao ametangazia radio okapi ya kuwa wameachiliwa bila hata kupewa pesa miya, akisema ya kwamba hawana uwezo wa kupata mahali pa kuishi na kuanza kujenga.

Aliendelea na kusema ya kuwa anafahamu wenzake zaidi ya 56 tayari wamejiunga na makundi ya wapiganaji wanao piganisha serikali ya Congo.

Uongozi wa kiraia huendelea na kusema ya kuwa viongozi wa ngazi za msingi wana hofu ya kuwa wapiganaji hao waweza kuzua mzozo wa kikabila na kusababisha usalama mbovu hata kama usalama haukuwa mwema zaidi katika wilaya hio.

Wapiganaji hao ni zaidi za 1.000 na waliwaleta katika wilaya ya Rutchuru baada ya miaka 3 wakiwa katika vituo vya mafundisho vya Kamina  huko Lualaba, Kitona  mjini Kongo-Central na  Kotakoli   ya jimbo ya Equateur.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[xyz-ihs snippet=”google”]

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.