kwamamaza 7

Rusizi:Wasiwasi kadhalika zazuka baada ya gari la wagonjwa kuharibika

0

Walowezi 20,250 wa wilaya ya Rusizi wanaotumia zahanati ya Nyabitimbo,tarafa ya Butare wana wasiwasi nyingi baada ya miezi 4 gari lililokuwa likiwapeleka wagonjwa kwenye hospitali ya Mibirizi, kuharibika.

Zahanati ya Nyabitimbo ambayo ni mbali na hospitali ya Mibilizi

Walowezi wametangazia Bwiza.com kuwa wana tatizo kubwa la kuwa idadi ya wazazi watakaokufa wakijifungua itaongezeka kwa kuwa wengi huishi mbali na zahanati  kwa umbali  kati ya km 27na 59  na kuwa wanatumia vifaa vya kienyeji kuwabeba wagonjwa kisha wakangojea masaa 9 gari la wagonjwa kutoka hospitali ya Mibilizi .

Wamendelea kwa kusema kuwa wanaishi katika hali mbaya ya kutokuwa na mabarabara safi ambayo wanasisitiza kuwa ndiyo chanzo cha gari la wagonjwa kuharibika na kuomba serikali kuwaletea gari jingine la wagonjwa kwa upesi.Mmoja wao Mukarugira Epiphania amesema”Gari la wagonjwa kutoka Mibilizi haliwezi kusaidia mzazi mja mzito baada ya kuenda km32 kwenye barabara zinazoja mashimo,mvuani ”.

Walowezi wa Rusizi ambao wanaomba msaada wa gali la wagonjwa

Akieleza kuhusu haya kiongozi wa takwimu wa zahanati ya Nyabitimbo,Ngendahimana Felix amesema kuwa gari hili ilianza kazi mwaka 2008  na kuwa lilizeheka na kusema  kwamba hawajafiwa mtu baada ya hili gari kufa lakini wazazi wanajifungua kabla ya kufika hospitalini.Haya ni maneno yanayosisitizwa na kiongozi makamu kwa wajibu wa mambo ya kijamii,Nsigaye Emmanuel  ambaye amesema kuwa ni tatizo linalohitaji msaada wa wizara ya afya.

Kiongozi makamu wa wilaya ya Rusizi kwa wajibu wa mambo ya kijamii,Nsigaye Emmanuel

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.