Swahili
Home » Rusizi:Ujauzito usio na mpango wasababisha watoto wengi kuacha shule
HABARI

Rusizi:Ujauzito usio na mpango wasababisha watoto wengi kuacha shule

wenyeji wa Rusizi wenye wasiwasi ya ujauzito usio na mpango wa watoto wao

Wazazi wa wattoto kutoka kijiji cha Rasano,tarafa ya Bweyeye wanasema kwamba wana wasiwasi ya idadi kubwa ya watoto wanaopachikwa mimba bila mpango na kuacha masomo.

wenyeji wa Rusizi wenye wasiwasi ya ujauzito usio na mpango wa watoto wao.

Wenyeji wa Kijiji cha Rasano  wanasema kuwa wanasema kwamba mbali hali yao ya ukufukara wanahofia ujauzito wa wanafunzi wa shule za msingi.Wanasema kuwa watoto hawa wajawazito hawana uwezo wowote wa kutoa uwezo wa mahitaji ya msingi.Sebujangwe Vianney ni mzazi wa miaka  59 amesema  kuwa mwanawe alipachikwa mimba alipokuwa akisoma kidato cha 5 na kuwa aligoma kuwaambia aliyempachika mimba kwa kusema”Binti yangu anatimiza miezi 6 baada ya kuzaa,alipokuwa mja mzito alitoloka na kukosekana na sasa hasomi,sina uwezo wa kulipa bima ya afya”.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mwenzake Ngirente Jeremie amesema kuwa na ye ana mtoto aliyezaa akisoma kidato cha 6 na kuacha shule bila kufanya mtihani wa serikali na kuwa alikosa la kufanya ili kumsaidia mtoto wake.Wazazi hawa wanasisitiza kuwa wahasherati ndio wanaharibu watoto wao kwa kuwapatia mambo ya kitoto kama vile rununu na mengine. Akieleza kuhusu habari hizi, katibu mtendaji wa tarafa ya Bweyeye,Sindayiheba Aphrodis amesema kuwa hili ni tatizo zito mno na kuomba wazazi kutoa  mchango wao.Aphrodis amesema”Hili ni tatizo kubwa ambalo linasababisha watoto kuacha shule lakini tunaomba wazazi wenye matatizo haya kuchukua nafasi ya kwanza kutusaidia”.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com