kwamamaza 7

Rusizi:Sekta binafsi yakosoa matumizi ya kituo cha magari cha Rusizi

0

Sekata binafsi wilayani Rusizi imekosoa matumizi ya kituo cha magari cha Rusizi kufuatia uchache wa miundo mbinu ,jambo linalopunguza mapato.

Kiongozi wa sekta binafsi wilayani Rusizi,Jean Bosco Ngabonziza amelezea Bwiza.com kwamba hali ya kituo cha magari cha Rusizi haipendezi kutokana na kuwa kuna mahitaji murua ambayo yanakosekana,jambo linasababisha utoaji wa huduma mbaya.

Pia Jean Bosco amependekeza wilaya kuwapatia rukhusa ya kuboresha kituo hiki kwa manufaa ya umma na kuwa inabidi kujenga nyumba nyingi za shuguli mbalimbali kwa kurahisisha utoaji wa huduma kwa watumiaji hasa wasafiri,madereva na wengine.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Katibu Mtendaji wa wilaya ya Rusizi,Ephrem Mushimiyimana amefafanua kwamba baraza la washauri wa wilaya walisha toa uamuzi wa kuweka kituo hiki mikononi mwa  sekta binafsi  ila kunasubiliwa wafundi ili kujua gharama ya kituo hiki.

Pamoja na hili,viongozi wa wilaya wameleza kwamba mradi wa kujenga kituo hiki uligharamiwa frw miliyoni 600.

Kituo cha magari cha Rusizi hutumiwa na watu wengi kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya pamoja na raia wa DR Congo.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.