kwamamaza 7

Rusizi: Shambulio la risasi lawauwa 1 na wengine 8 Kujeruhiwa

0

Shambulio la watu wenye silaha waliofyatua risasi lamuua mutu 1 na kuwajeruhi wengine 8 katika tarafa ya Bugarama, wilaya ya Rusizi karibu na mpaka wa Rwanda na Burundi.

Kulitokea shambulio jingine lililowafanya watu wengine 2 kupoteza maisha katika eneo hili miezi michache iliyopita washambulizi hawa walidhananiwa kuwa walikuwa wanatoka nchini Burundi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Shambulio hili limetekelezwa na watu wasiojulikana bado kwa mjibu wa habari alizoitangazia Rediyo Rwanda, Lt. Colonel René Ngendahimana Msemaji wa Jeshi la Rwanda. Amesema kwamba shambulio hili limemuua mtu mmoja na kuwafanya wengine 8 kujeruhiwa na wamepelekwa hospitali kwa matibabu. Upelelezi wa kugundua chanzo cha shambulio hili na wahusika wake umekwisha anza.

Aidha kuna habari nyingine zisemazo kwamba shambulio hili limewafanya watu wasiopungua 7 kupoteza maisha.

Meya wa Rusizi hakutangaza mengi kuhusu shambulio hili na akasema kwamba wanalifuatilia kwa karibu tukio hili na watatupasha habari zaidi baadaye kuhusu chanzo chake na waliohusika.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.