kwamamaza 7

Nyamasheke: Radi ilio shituwa wengi ilirarua mjamzito akiwa nyumbani mwake

1

Tarehe 1 Mach 2017, mvua ilinyesha ila bila upepo mwingi na radi katika kata ya Ruharambuga, kiini ya Nyamasheke, kijiji ya Kamabuye, ila kwa gafla radi ilipiga kwa sauti kubwa karibu watu wengi wakatishwa na ikapituwa mama mjamzito wa miezi 6 na akafariki akiwa nyumbani mwake.

Mukamana Emmanuella alisema ya kuwa yalifanyika karibu saa tisa na dakika kumi za jiani wakati wa mvua nyingi, ndipo radi ilipiga na dakika chache ndipo wakasikia ya kuwa mama huo mjamzito mwenye umri wa miaka 32 amepigwa na radi akaaga dunia.

Aliendelea na kusema ya kuwa habari hio mbaya iliwafikiwa wakiwa kwenye kikao cha kata wakati mvua ilikuwa ikinyesha kama kawaida na alisema ya kuwa karibu ya wote walio kuwa hapo walishitua na pigo la radi hio.

Marehemu alijulikana kwa jina la Mateso Esperence, na mwili wake ulichukuliwa kwenda hospitali ya Bushenge ili kuachanisha mzazi na mtoto anayekuwa tumboni ili waweze kuwazika kikawaida.

Uongozi wa kata umeomba raia kujiadhali na radi kwa wakati huu wa mvua na kutii maelekezo wanao pewa na viongozi kwa ajili ya wakati huu wa mvua mwingi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Tarehe kama hii mwezi nenda katika kata jirani ya Giheke, wilaya ya Rusizi radi iliua ng’ombe 2, kondoo 6 zote za jamii moja na kujeruhi vikali msichana mwenye umri wa miaka 18.

Marehemu amemuacha mume na watoto 3 wakati alikuwa akijiandaa kuzaa mtoto wa inne na mazishi ni leo alhamisi.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com,chanzo:imvaho

1 Comment
  1. Mudris Msodoki says

    Pole sana jamaa wa mzazi huyo mungu amlaze pohalapema.

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.