Swahili
Home » Rulindo na Nyarugenge ndizo wilaya zilizompokea mgombea wa chama cha RPF Kagame
HABARI MPYA SIASA

Rulindo na Nyarugenge ndizo wilaya zilizompokea mgombea wa chama cha RPF Kagame

Leo, ikiwa ni siku ya 7 ya kuendesha kampeni za urais kwa wagombea wanaowania kiti cha urais katika uchaguzi utakaofanyika mwezi ujao mgombea wa chama cha RPF amekuwa kwenye wilaya mbili ambazo ni Rulindo na Nyarugenge.

Katika kampeni ya leo ambako kumekuwa wananchi wengi sana na viashiria na vibandiko vingi vya RPF.

kwenye Kilima-Rulindo

Mwenyekiti wa chama kilichojiunga na RPF cha PSD, Vincent Biruta, ndiye aliyeanza kuhotubia na kusema kwamba wana urafiki wa kudumu miaka 25 na kusema kwamba wanaunga mkono mgombea wa chama cha RPF kwamba ni nguzo ya umoja,demokrasia na maendeleo.

 

Aliendelea kusema “mgombea wetu ndiye wa kufa, anaposema ndivyo atendavyo na hiyo tulikwisha jionea umeme umekwisha fikia 26% na mengine yangali njiani”

Mwenyekiti wa PSD Vincent Biruta

Mh. Paul Kagame ndiye aliyefuata kuhotubia akieleza mipango yake kwa wananchi wa Rulindo na kuwaahidi yale atakayewatendea. “mnajua vita vilivyotokea hapa lakini kwa sasa hakuna ishara ya hayo lakini hilo silo tunalolitaka. Tuyonataka ni shughuli za kilimo na ufugaji, madarasa, na miundombinu.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Hakuna yeyote ambaye angethubutu kuharibu yale tuliyojenga tukikunja mikono tu”

Kagame aliwakumbusha kuwa tarehe 4 Agosti ndio tarehe ya kuamua ikiwa wataendelea kujenga nchi ambayo ni safari wanaofanya kwa pamoja kutoka muda mrefu.

Alisema kuwa pia wamemfurahisha na kwamba yuko tayari kuendelea pamoja nao ikiwa watampa kura katika uchaguzi.

Baada ya hapo aliendelea na shughuli zake wilaya ya Nyurugenge mjini Kigali

Akiwa kampeni kwenye wilaya ya Nyarugenge

Baada ya wanachi kumpokea kwa wingi hapa tofauti na wilaya ya Rulindo mwenyekiti wa chama cha PDI ndiye aliyehotubia na kumshukuru rais Kagame kwa yale aliyoyafanya na kwamba alirudisha Kiswahili miongoni mwa Lugha halali na kwamba aliwapa uhuru waamini wa dini tofauti na hali wakati wa kikoloni.

Wanachama waliojiunga

Paul Kagame alipoanza hotuba yake alirejea kwa yale mwenyekiti wa PDI aliyokwisha sema kwamba yanamkumbusha historia ambayo Rwanda ilipitia na kwamba mpaka sasa watu wamebadilika moja hakuna, muislam, mkristo na wala wenye kabila lolote .

Hapa aliongeza kwa ni nguvu za pamoja za RPF na wananchi na hata vyama vilivyojiunga.

Akiongea kuhusu uchaguzi alisema “tarehe nne ni ina maana ya kuongeza nguvu, kasi mwa yale tunayoyafanya. Tuendelee na usalama,umoja, umeme na elimu vya kudumu.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Alikamilisha hotuba yake akiwashkuru kwa kuhudhuria kwa wingi na kusema kuwa wanachoweka mbele ni maendeleo yasiyomwacha yeyote nyuma na kwamba vijana wanalazimika kuongeza nguvu kwenye shughuli zake za maendeleo.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com