kwamamaza 7

Rubaya: Pombe haramu, ugomvi bila kuhasau kupigwa fimbo

0

Katika kata ya Rubaya wilaya ya Gicumbi, husema hakuna hata wiki bila kusikia ugomvi na kupigwa fimbo, kiongozi akiwapiga raia, wanaume wakiwapiga wake zao, wano piga pombe haramu (abarembetsi) nao wanawapiga wanao linda amani, nao hufikishwa kwa wenye kuhusika na usalama.

Tangu mwaka huu kuanza, vitendo vya ugomvi vilisemwa sana sehemu hio, na sehemu ijulikanayo kwa jina la Rusambya mwanamke anaishi na ulemavu ulio letwa na mume wake, na kila siku yupo na vidonda kutoka fimbo anazo pigwa. Na inajulikana ya kuwa katika kiini ya Gishari raia waliiba bendera ya nchi mara mbili.

Mwanzo wa mwezi huu, raia walisema ya kuwa kiongozi wao wa kata yupo na uzoefu wa kuwapiga wakitoa mfano wa watu sita kama vile husema gazeti umusingi, na kiongozi alikubali ya kuwa anawapiga wa sababu wanakataa kwenda kwa kazi ya umma na tena waliiba bendera ya nchi na kuikata vipande.

Wiki hii wafanya biashara ya pombe haramu wajulikanao kwa jina la “abarembetsi” pia walipiga wafanya usalama wa msingi na kuwatesa na wanafananishwa na wengine wenye kuishi kata ya Cyumba wajulikanao kwa jina la “abahubuzi”, wao huhusika na kuiba na ugomvi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kata za wilaya ya Gicumbi ambazo ni kando ya nchi jirani Uganda wote wako na hilo tatizo la pombe haramu, na wengi huvuka ngambo wanarudi wakiwa walevi wa hali ya juu, na kata hizo ni kama Manyagiro, Cyumba, Kaniga, Rushaki ingine ikiwa ya wilaya ya Burera na Kivuye, Bungwe.

Kiongozi wa kata ya Rubaya Nkunzurwanda anasema ya kuwa dawa moja ya kulevya inayo wasumbua ni pombe hio haramu na matokeo ni ulevi, ugomvi na uzinifu na kuzaa watoto wengi bila malezi.

Baada ya Warembetsi kuwapiga wanao husika na usalama wa msingi, viongozi wa ngazi tofauti pakiwemo kiongozi wa jimbo ya Kaskazini Musabyimana Jean Claude, kiongozi wa jeshi Br.Gen Nkubito Eugene, kiongozi wa polisi  ACP Mutezintare Bertin  na kiongozi wa wilaya ya Gicumbi Mudaheranwa Juvenal walitembelea kata hiyo,

Br. Gen Nkubito, alisema ya kuwa wale wote hufanya ugomvi utokanao na kunywa hio pombe haramu (kanyanga) na kufikia hali ya kuwapiga walinzi wa usalama wa msingi, hao kuchukuliwa kama adui wa nchi.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.