kwamamaza 7

Rubavu:Wafanyabiashara kwenye soko la Gisenyi wakumbwa na hasara kwa sababu ya mvua inayowanyeshea

0

Wafanyabiashara kwenye soko kukuu la Gisenyi wametangaza kupata hasara  kwa sababu ya mvua inayowanyeshea kwa kuwa soko hili hakuna paa.

Wafanyabiashara wametangazia VOA kwamba mvua inanyeshea bidhaa zao kama vile sukari,chumvi,sabuni na mengine hasa majira ya mvua kali ya siku hizi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mmoja wao amesema kuwa bidha zake kama sabuni,unga zinaharibika kwa kuwa anatumia mwavuli mkubwa ili kulinda bidhaa zake na kuongeza kwamba  hajui namna gani serikali ilishindwa kuwajengea soko wakati ambapo wanalipa kodi za serikali kila mwezi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pamoja na haya,kuna soko linalomaliza miaka sita kwa kujengwa bila kumalizika.

Mkurugenzi wa soko la Gisenyi,Jean Bosco Uwimana amethibitisha taarifa hizi kuwa wafanyabiashara wananyeshewa na mvua na kuwa kunasubiriwa kumaliza kazi za kujenga soko mpya la gorofa sita.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Diwani wa mpito,Janver Murenzi amesema kuwa anajua suala hili na kuwa mradi wa kujenga soko mpya ulichelewa kwa kuwa kulijitokeza kutoelewana kati ya kampuni ya kulijenga,HABA Ltd na wilaya,jambo lilifikisha kesi hii mahakamani.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Hatimaye,kuchelewa kulijenga soko hili kulifanya wilaya ya Rubavu kupata nafasi ya mwisho kwenye mkataba wa utendaji wa mwaka 2016/2017.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.