Swahili
HABARI MPYA

Rubavu:Njaa yavuma baada ya wilaya kuzuia wenyeji kuchimba mchanga.

Wachimbaji wa mchanga katika wilaya ya Rubavu.

Njaa inangamiza wenyeji 3,000 wa wilaya ya Rubavu baada ya viongozi  kuwakataza kuchimba mchanga mtoni Sebeya,kufinyanga matafari kwa kuwa kazi hizi zilikuwa ni asili ya kujipatia chakula.

Wachimbaji wa mchanga katika wilaya ya Rubavu.

Wenyeji wanasema kwamba kitendo cha viongozi wao kinasababisha njaa kwa kuwa kazi hizi zilikuwa zikiwawezesha kupata fedha kila siku na kuwa hawajui sababu ya viongozi wa wilaya kuzikomesha.Akizungumza na Bwiza .com mmoja wao,Uwase Clemence amesema kuwa tukio hili lilimzuia pato lake la fedha 1500 za kila siku kwa kusema”Nilikuwa nikipata faranga 1500 kila siku na kuweza kujilipia mituweli,chakula”.

Jambo hili lasisitizwa na wa wafinyanzi wa matafari wanajiuliza kwa nini viongozi waliamua bila kuwauliza ili watoe michango yao kimaoni na kuwa hawakupatiwa hati rasmi ya serikali.Mmoja wao Kanyange Alphonse yaeleza kuwa walishtuka kusikia habari hizi na kuwa ni hatari sana kwa maisha yao akisema”Tulishanga kusikia habari hizi,hili jambo linaathiri maisha yetu”.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Menyeji huyu ameongeza kwamba hawataweza kulipa madeni ya benki na kuomba msada wa serikali kwa kuwa kazi  zao zilikuwa zikiwasaidia sana.Kwa upande wa serikali kiongozi makamu wa wilaya kwa wajibu wa fedha na maendeleo,Murenzi Janvier amekubali kuwa kuna waliokomeshwa milele na waliokomeshwa kwa mda mfupi na kusema”Ni ukweli tuliwakomesha kwa kuwa wanafanya kazi yao  bila mpango,kwa ghasia,bila hati  rasmi za REMA”.

Wenyeji hawakubali madai ya kiongozi wao kwa kusema kwamba waliomba hizo hati miaka nenda rudi bila kupatiwa.Kunahesabiwa mashirika 11 anayochimba mchanga na mengine anayofinyanga matafari katika wilaya ya Rubavu.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Fred/Bwiza.com

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com