kwamamaza 7

Rubavu:Mvua kali yaharibu nyumba 926

0

Mvua kali iliyonyesha katika tarafa ya Rugerero na Migeshi wilayani Rubavu kaskazini magharibi mwa Rwanda imetokomeza nyumba 26 na kubomoa angalau nyumba 900na vyooni 254 kutokana na maji ya mto  Sebeya.

Wakazi wa eneo hili wametangaza kupoteza mali yote iliyokuwa katika nyumba zilizoharibika na kuwa wanahitaji msaada ili maisha yao yaendelee kama kawaida.

“Yote yameharibika nimeweza kunusuru vitu vichache,tunahitaji msaada”mmoja amesema

Gavana wa mkoa wa Magharibi,Alphonse Munyentwari ameeleza kuwa leo serikali  inajianda vilivyo kuwasaidia wakazi.

“Tumefanya mkutano kuchunguza namna ya kutoa msaada hasa vifaa pamoja na MIDIMAR,Croix-Rouge Rwanda”.

Viongozi wa hospitali ya Gisenyi wametangazia RBA kuwa watu wanne walijeruhiwa ila hawakukubali watangazaji kuwatembelea hawa wagonjwa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pengine mvua hii imeharibu mazao ya wakazi pamoja na ha 18 za chai.

Gavana ameongeza kuwa serikali ilianza mradi wa kuhifadhi chimbuko la mto  Sebeya lililoko wilayani Ngororero ili kujikinga majanga yanayosababishwa na huu mto.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.