Swahili
HABARI

Rubavu:Mafisa wa mpaka wafichua siri ya ufanyabiashara marufuku

Mafisa wa mpaka kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia  ya Congo,wilaya ya Rubavu wamefafanua namna ambavyo ufanyabiashara marufuku unaongezeka kutokana na kuwa hakuna jambo wazi la asiri kati ya nchi hizi kama vile mto,miti na mengine.

Wakizungumza na Bwiza.com wamesema kwamba mbali na haya,miongoni mwa mafisa wa pande zote mbili hupokea rushwa kisha bidhaa marufuku kama vile bangi,dawa za kulevya zikaingia nchini Rwanda.Mmoja wao,Mawazo Oliva amesema kuwa rushwa ndiyo chanzo cha haya na kusema”Rushwa inaendelea hapa kwenye mpaka lakini kupitia kisirisiri”.

Kwa hiyo,viongozi wamekusanyika katika mkutano na kufichua siri za ufanyabiashara marufuku zikiwemo kuficha bangi katika nywele,viatu,mgongoni,ugalini,katika maboga na kadhaa.Akiwongea na washiriki,Kiongozi kwa wajibu wa uhamiaji mkoa wa magharibi,Gatarama Benois ameongeza kuwa kuna mbinu kadhalika za wafanyabiashara marufuku na kuomba polisi kutumia mbwa wa kuchunguza madawa ya kulevya na silaha.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Akizungumza kuhusu haya,afisa wa wiziara ya Afrika mashariki(MINIACOM),Tayobwa James amesema kuwa wanahamasisha wakazi wa eneo hili kuacha ufanyabiashara marufuku na kuwa kutakuweko ushawishi kwa serikali ili wapate kazi za kufanya.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com