Swahili
HABARI

Rubavu:Familia 24 waliofukuzwa Tanzania wanung’unikia hali ya maisha yao

Raia wa Rwanda waliofukuzwa nchini Tanzania na kuhamishwa tarafa ya Cyanzarwe,wilaya ya Rubavu wanalalamika kwa kuwa hawana furaha kulingana na hali ya maisha yao.Malalamishi yao yanasababishwa na kuwa hawakupatiwa vieti vya nyumba na mashamba waliyopewa na serikali na hata wanjaeshi wanawakataza kulima mashamba yao.

Raia hawa walihamishwa nchini Rwanda mwaka 2014 baada ya kufukuzwa nchini Tanzania. wanasema kwamba hali ya maisha yao haipendezi baada ya wengi wao kukataliwa msada wa fedha za Vision Umurenge Program(VUP).

Hii ni hali waliyo mueleza mtangazaji wa radiyo Sauti ya marekani wakisema kuwa wanaishi kwa kukiukiwa haki za kulima mashamba waliyopewa kama asili ya kujitunza.Mmoja ameleza”Tuna changamoto ya kuwa shamba tulilopewa ilikuwa inaambatana na Congo,tukienda kulima wanajeshi hutukataza wakisema kuwa hawaamini usalama wa maisha yetu”.Mwenzake amemuambia mtangazaji kuwa maisha yao hayana msimamo kwa kuwa na  hawakubaliwi kulima mashamba yao na wakijaribu wanapigwa.

Raia hawa wameendelea kusema  kwamba walilima msimu wa kilimo uliopita baada yaw engine na kwa kuwa waliolima hawakuweza kupalilia au kufuatilia mazao yao kwa kuwa hwanajeshi wanawakatalia kuenda kulima mashamba yao.Kwa upande wa uongozi wa jeshi la Rwanda, spika wake Brig.Gen.Ferdinand Safari amesema habari hizi ni fununu na kusema”Kumbuka kwamba mwaka wa 2015 kulitokewa upenyezi,hilo ndilo jambo moja tuliliowahi kuwakataza kuenda kulima ili kujilinda matata”.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Spika huyu wa RDF ameeleza kuwa habari mpya ziizotangazwa na raia hawa ni kuwa wanakubaliwa kulima angalau siku mbili wiki moja.Amesema kuwa jambo murua ni kuwa serikali inagli tayari kuwasaidia na kuwa usalama unavuma sehemu hiyo.Tena kiongozi makamu wa wilaya ya Rubavu kwa wajibu wa jambo kijamii,Uwampayizina Grace amesema kwamba ni mala ya kwanza masikioni mwake kusikia kuwa wanajeshi wanakataza raia hawa kuenda kulima mashamba yao.

Mwanajeshi akitoa msada wa kujenga nyumba ya raia wa Rwanda aliyefukuzwa tanzania

Ameeleza”Sijui kuwa wanawarudisha lakini nafikiri kuwa mada hii inawahusu sana wana usalamayawezekana kuwa ni mbinu za kujilinda adui kama mnajvyojua FDLR huishi karibu nasi”.

Familia hizi 24 zilihamishwa kijiji cha Busigari,tarafa ya Cyanzarwe wanaishi katika nyumba ambazo hazikusafishwa vilivyo kwa kuwa nyingi zilisafishwa upande wa nyuma tu.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com