kwamamaza 7

Rubavu:Bei ya usfirishaji yaongezeka kiholela

0

Wasafiri wa mjini Gisenyi,kaskazini magharibi  mwa Rwanda wametangaza kuwa na tatizo la madereva wanaotaka kulipwa nauli zaidi ya ile ya kawaida hasa majira ya jioni.

Mmoja wao Clement Muyombano ametangazia Bwiza.com kwamba nauli inaongezeka mno hususani jioni

Kwa kawaida tunalipa frw 300 kutoka Gisenyi kuenda Mahoko, Nyakiriba lakini siku hizi tunalipa kuanzia frw 400-100 hasa saa za jioni”ameleza Clement.

Mwenzake Adidja Nyiraneza ameeleza kwamba mbali na kuwachelewesha kuna wakati ambapo wanawacha njiani.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kwa upande wa madereva wa mjini  Gisenyi,wamehakikisha taarifa hizi na kuwa wanaongeza nauli hasa jioni kwa kuwa wasafiri huwa wengi mno.

Afisa wa shilika la usafirishaji(RFTC)wilayani Rubavu,Antoine Karenzi amesema kwamba tatizo hili linajulikana na kuwa hairuhusiwi kuongeza bei kiholela.

Bw Antoine Karenzi ameongeza kwamba kunajadiliwa namna ya kupambana na tatizo hili na kusisitiza kwamba nauli ya kawaida iliotolewa na RURA ni frw 300.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.