kwamamaza 7

Rubavu: Uingi wa wanafunzi darasani pingamizi kwa elmu ubora

0

Wastani ya watoto 140 ndio wanaotumia chumba kimoja huku wakigawika kwenye makundi ambapo kundi moja linapishana muda na wenzio ashubuhi na baada ya saa sita hivyo hivyo.

Miezi mitatu ilikwisha kamilika huku wanafunzi wa darasa la nne wa Shule la Msingi la Buhaza wakisomea nchini ya jua kali, na wakati wa mvua wakajikinga kwenye mabaraza. Hayo yote kutokana na uhaba wa vyumba vya shule ambapo shule hili linahudumia jumla ya watoto 1260 likiwa na vyumba tisa tu!

Kwa sasa kuna namna ya nafuu baada ya kuazimiwa vyumba kutoka shule lililokuwa Lycee de Gisenyi vinavyomilikiwa kwa sasa na chuo cha kujitegemea la UTB.

Mkurugenzi wa Shule la Msingi la Buhaza, Niyontego Kagaba Vincent, alitangaza kwamba kwa sasa mambo yanaendelea vizuri baada ya kuazimwa vyumba hivyo vya madarasa, lakini pia akajiwaza hali itakuwaje baada ya wamiliki wa vyumba hivyo vya madarasa kuchukua vyumba vyao.

“viongozi wa wilaya(inaongozwa na meya Sinamenye), ndio wanafahamu kwa kuwa wajibu ni wao. Wakitutoa nje tutatoka” Mkurugenzi alisema.

Aliongeza kwamba masomo yenye kutolewa nje ya madarasa hawezi kuenda vizuri, kwa maneno machache “ni hivyo tu huwa tuna wasiwasi”

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mmoja wa viongozi wa ngazi ya Wilaya aliarifu kwamba kuna mpango wakujenga vyumba vya darasa viwili kwa ajili ya Shule hili, na kusema kwamba maandalizi ya fedha na vifaa yamekwisha.

La hasha amemshutumu Mkurugenzi wa shule hili kwa kutotoa taarifa kwa wakati, kwa kuwa wilaya ilijenga vyumba 2 na kwa kushirikiana na wazazi wakajenga chumba kimoja zaidi.

Hii ndio sababu ya kushtumu Mkurungenzi wa shule kwa kusababisha tatizo hili kwa kutofafanua tatizo hili. Amemshtumu pia Mkurugenzi huu kuwasajili watoto zaidi ya uwezo wa shule na hatoi tarifa ili waweze kuhamisha watoto wa ziada kwa shule jirani.

Habari hii ni ya kuaibisha kuona tatizo la watoto wangali wakisomea nje wakiwakiwa na jua na mvua ikiwanyeshea. Serikali imekuwa ikifanya jitihada kutolea suluhu tatizo hili kwa kuwa hadi sasa kunahesabiwa ongezeko kubwa la vyumba vya darasa nchini kote ikiwa lengo ni kufikia idadi ya wanafunzi 24 kwa mwalimu.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.