kwamamaza 7

Rubavu: Raia wasiojiweza waliootoka uhamishoni kutoka Kongo wapewa nyumba

0

Tarehe 1 mwezi wa Juni , Sehumu za Ndoranyi , kijiji cha Nyabishongo, taarafa ya Mudende kumekuwa sherehe ya kuzindua hadharani nyumba 6 kwa ajili ya familia za wanyarwanda waliotoka uhamishoni kwenye Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa madhumuni ya kustawisha maisha yao.

Raia hawa waliopewa nyumba hizi ambazo kila moja iligharimu milioni ya faranga za Rwanda walisema kwamba wanashkuru serikali inayomjali kila mwananchi bila mapendeleo yoyote. Wengi miongoni mwao walitoka uhamishoni baada ya 2014.

Raia mojawapo, anayeitwa Musabimana Phillipe, alisema kwamba alihamia Kongo na familia yake, walipofika hapo wazazi wake walifariki badaaye na ilimbidi kuishi maishi mabaya. Kwa bahati nzuri alipotoka uhamishoni serikali ilimsaidia kujifunza masomo ya kazi za mikono, na wakamsaidia kuanza biashara ya kibinafsi, na anafuraha ya kwamba zaidi ya hayo yote wamempatia nyumba ya kuishi.

Alisema “Nilipofika Rwanda nilipewa msaada wa mwanzo ambao niliona kuwa wa kuridhisha lakini zaidi ya hayo wamenipa pia nyumba ya kuishi, kwa hivi nashkuru serikali ya Rwanda ambayo inatawaliwa na rais Paul Kagame”

[xyz-ihs snippet=”google”]

Raia wengine vilevile walipata fursa ya kuwaitia watu ambao wangali uhamishoni katika misitu ya Kongo kurudi nchini mwao nakunufaika na sera na mambo mazuri serikali inayowaletea raia wake bila mapendeleleo ya namna yoyote kama inavyoelezea taarifa hii kutoka gazeti la Imvaho Nshya.

Waziri Mukantabana Seraphine, wa Wizara ya Kuwatetea Wakimbizi na Kupambana na Majanga, alisema kwamba nyumba hizi zilijaa zikigharimu milioni 42 ya faranga za Rwanda, na waliwajengea kwa kuwa waliona hawana uwezo, ni ilikuwa ni kulingana na mfumo wa kuwasaidia kupata malazi, aliwakumbusha pia kwamba wana wajibu wa kumpambania maendeleo yao binafsi.

Alisema “ serikali imewajengea nyumba imara za kisasa na zinazoweza kuthubutu majanga . Ni zamu yenu kuzitunza sasa na kuzizalisha mali, mnapaswa kufanya bidii ili mweke vifaa vingali kosekana , hamruhusiwi kuuza mnapaswa kusukua, Hii ni sawa na jinsi rais anavyowapenda”

Kwa sasa kumeishajengwa nyumba 115 kwa ajili ya malazi ya watu waliotoka uhamishoni mwa nchi mbalimbali na imefikiwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Wakimbizi na Kudhibiti Majanga na idara ya malazi ya watu ″UN Habitat″ ya Umoja wa Mataifa.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.