kwamamaza 7

Rubavu: Mwezi umekwisha pita bila kushafisha soko la Mbugangari

0

Viongozi wa soko la Mbugangari watangaza kwamba mwezi umekwisha pita chama cha ushirikiano cha uchukuzi wa michafu kikifunga milango na kufanya matuta ya uchafu kuundika katikati ya soko na kuwakera watu .

Kama alivyotangaza Yussuf Saiba, Kiongozi wa soko hilo tangu tarehe 3 mei 2017 shirika la KOPIBU( Koperative Isuku kuri Bosi) halijatokea hata wakati mmoja kuchukuwa michafu kwenye soko hilo, licha ya kwamba wanaarifu ngazi husika siku hadi siku bila kupata jibu. “Tulimwarifu katibu mtendaji wa tarafa na eneo na tuliaarifu viongozi wa shirika hilo lakini jibu hatukupata ingawa kandarasi na wilaya inawapasa kuchukua michafu kila siku”

Uchafu huu wa kuzidi kwenye soko hili na maeneo karibu yake ni changamoto kwa wakaazi wa eneo hili ambao mojawapo wanasema wana wasiwasi kuwa utawaambukiza magonjwa. Mukamana Jeannine asema “ Kuna nzi wa kupita kiwango, hakuna yeyote anangethubutu kupata chakula kwenye restorenti za hapa karibu, watusaidie kabisa”

[xyz-ihs snippet=”google”]

Bwiza.com ilimhoji kiongozi wa shirika hili na kutwambia kwamba wanadaiwa na Wilaya faranga zipatazo milioni 8, na hii imewafanya wafanyakazi wa shirika hili kufa moyo kwa kotolipwa.

Kiongozi makamu wa Shirika hili, Ndagijimana Innocent alisema “ingawa viongozi wa soko hili wanasema kwamba mwezi umekwisha pita bila kuchua michafu, kungetokea wakati tukaja kuchukua michafu, kutokuja kuichukua ni kwa sababu miezi mitanu imekwisha pita bila wilaya kutulipa wakati ambapo wanatarajiwa kutulipa milioni moja na laki saba ya faranga za Rwanda, tuna wafanyakazi 30”

Hili ni suala ambalo tunalijuwa na tunafanya kila iwezekanayo kulitatuwa punde si punde siyo baada ya leo litakwisha ,suala lenyewe lilisababishwa na viongozi wa shirika hili, tulikaa pamoja na kulijadili na kuna matumaini litatatuliwa hii leo”

Ingawa hataji chanzo cha ufanyaji kazi mbaya, anasema kuwa suala hili litapatiwa suluhu. La hasha ,Si rahisi kupata suluhu la suala ambalo limekaa miezi mitano bila jibu”.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.