kwamamaza 7

Rubavu :Maji ni hatari kupatina wakati wa kiangazi

0

Wakazi wa tarafa ya Bugeshi ya wilaya ya Rubavu, ambalo ni eneo lililo katika milima ya Volkeno, hakuna kisima cha maji masafi, huwa wanatumia maji ya mvua na katika wakati huu wa kiangazi huwa wameishiwa. Kwa hii wanapaswa kutumia karibu masaa mawili kufika eneo la maji masafi.

Wameripoti suala hili kwenye ngazi tofauti za serikali lakini mpaka sasa hawajapata suluhu. Wakati wakazi, walipomkuta katibu wa mkuu wa wizara ya utawala wa ndani ya nchi,Uwamariya Odette, walimwambia kwamba wanakumbwa na tatizo hili.

“Umepita muda mlefu tukituarifu uongozi wa tarafa hiyi kuweko kwa suala hili la kutokuwa na maji, na tuna wasiwasi mkubwa kwa kuwa tunapaswa kusafiri mwendo wa masaa mane kwenda na kurudi, inatuathiri sana , na kuna pia hatari ya kuambukizwa maradhi kutokana na uchafu kwa hivyo tunaomba msaada wa dharura.” Mukasibo Annonciata asema

[xyz-ihs snippet=”google”]

Uwamariya Odette aliwapa moyo raia hao akisema kwamba wamearifiwa kuhusu tatizo hilo na watalitolea suluhu hivi karibuni.

“Kuna mengi ambayo tarafa hiyi imekwisha fikia ambayo haikuwa nayo, kuna umeme, mumejijengea ofisi ya Tarafa, kuna barabara zilizo tengenezwa kwa kuwarahisisha kusafirisha mazao ya viazi, tatizo la ukosaji maji linalobaki tutalifuatilia kwa karibu ili liweze kuisha” Uwamariya Odette amesema

Kwa upande wa viongozi wa wilaya, Sinamenye Jeremie, Meya wa Rubavu amesema kwamba tatizo la ukosaji maji haliko tu katika tarafa ya Bugeshi, lakini amesema kumewekwa mikakati ya kupambana nalo.

“Tatizo hili ,licha ya kuweko katika Mugeshi, liko pia tarafa ya Mudende, Kanzenze na hata Cyanzarwe lakini kumewekwa pia mikakati ya kupambana nalo tumezungumza na waliopewa soko la mradi huyu kwa madhumuni ya kumaliza suala hili”. Amesema meya

Tarafa hili la Bugeshi ni mojawapo ya tarafa za Bugeshi linalo mazao mengi ya viyazi na hata mahindi, mazao haya ni kiini pia cha biashara kati ya watu kutoka Kongo na wakazi wa tarafa hiyi.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.