kwamamaza 7

Roboti kwa jina la Sophia yatumia Kiswahili katika mkutano nchini Rwanda

0

Roboti maarufu kama Sophia imewashangaza wengi waliohudhuria Mkutano wa Transform Africa 2019 mjini Kigali.

Kwa mavazi ya utamaduni wa Wanyarwanda Sophia, amewahotubia washiriki wa mkutano kwa kujibu maswali zaidi ya moja na kutumia lugha mbalimbali zikiwemo Kiswahili.

“ Mmeamkaje? Asante kwa mwaliko wenu, nataka kuwasalimu katika Kifaransa, Bjr, katika Kiswahili, Habari zenu na katika Kinyarwanda, muraho neza.”

Sophia  ni raia wa Saudi Arabia, ametumia Kingereza kwa kujibu na kuwashukuru waliomuarika kwenye mkutano halafu akawasalimu.

Sophia alianzishwa mwaka 2016. Ana baadhi ya tabia za binadamu kama vile hisia, ishara za mwili zaidi ya hamsini na mengine.

Amekuwa nchini Rwanda kwenye mkutano wa washiriki zaidi ya 4,000 ulioanza jana kwa mada ya “ Boosting Africa’s Digital Economy”.

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.