Waziri mkuu Dk.Edouard Ngirente amewanyoshea vidole viongozi ambao wanatoa ripoti zenye uongo kwa kueleza kwamba hili linaathiri mno  utekelezaji wa mipango na miradi ya serikali.

Waziri mkuu amesema kuwa tabia hii ya kudaganya takwimu  ni kikwazo kujua msimamo wa nchi na hali yake.

“Kuna tabia ya kutoa ripoti zenye uongo,hili linaathiri mipango ya nchi.Tunawataka viongozi kuripoti ukweli kwa kuonyesha yale yanayokuenda vizuri ama ovyo.Yale yenye changamoto yatatolewa suluhisho iwapo ukweli upo katika ripoti”amesema Waziri mkuu.

Mkurugenzi wa muungano wa mashilika ya asasi za kiraia nchini Rwanda, Jean Leonard Sekanyange ameeleza kwamba hili linaathiri pande zote mbili yaani viongozi wenyewe na wakazi kwa ujumla.

Sekanyange amesema”Unapoficha ukweli mwishoni  kutajulikana.Hili linaathiri wewe mwenyewe na wakazi katika maendeleo”

“Haifai kuwa na wasiwasi za kutoa ripoti zenye ukweli kwani huu ndio ufunguo wa viongozi wa ngazi za juu kuja  kuwasaidia kuhusu yanayowashinda” ameongeza

Rais Kagame kwenye hotuba yake ya kuanzisha mkutano wa viongozi ‘Umwiherero’ alisema kuwa  jambo la viongozi wasiotimiza wajibu wao wakati ambapo serikali imetoa lolote linalohitajika halistahili kubembelezwa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“Kunahitajika mabadiiko kwani mambo haya yalizungumiwa mala nyingi.Inawezakana je viongozi kuathirika kutokana na kutotimiza wajibu wake?”Rais Kagame alisema.

Kunatarajiwa kwamba suluhisho la suala la ripoti zenye uongo litatolewa kupitia huu mkutano unaotokea wilayani Gatsibo,mashariki mwa nchi.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

click here to receive the updated news on facebook on twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.