Taarifa husema ya kuwa wapiganaji wa chama cha FRPI (Force de résistance patriotique de l’Ituri) usiku wa juma inne walishambulia kambi la jeshi la Kaswara mangharibi mwa Bunia, wakaua wana jeshi wawili wa serikali la Congo na wakamuchoma kwa mtoto akiwa hai.

Shambulio hilo lilikua karibu saa mbili za usiku , na wapiganaji hao walikuwa na siliha na walikua wakifyetulia wana jeshi wa FARDC sehemu iitwao Kaswara katika Boloma.

Wana jeshi wawili waliuawa kama vile huhakikisha kiongozi wa Walendu Bindi na baada ya mapambanao hayo, wapiganaji hao walichoma pia kambi za jeshi ambazo zilikuwa kati ya Mogbe na Kaswara, taarifa kutoka redio Okapi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Hapo Kaswara mtoto wa askari jeshi alitupwa katika moto na wapiganaji na akaungua akiwa mzima, mwengine mke mwenye umri wa miaka 30 alijeruhiwa na risasi vikali.

Msemaji wa FARDC jimbo la Ituri, Capt. Kalombo Carlos, amehakikisha ya kwamba askari wawili walipoteza maisha, ila anakana ya kuwa walishambulia kambi la jeshi, anasema ya kwamba ni mtego waliotega wana jeshi wenye kulinda usalama, pia anakana ya kuwa mtoto alitupwa katika moto akiwa hai.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.