kwamamaza 7

RDC: Wanyamulenge wakabili vita vikali na Mai- Mai, serikali ikikaa kimya!

0

Watu wapatao wanne wamejeruhiwa katika vita vilivyowakumbanisha kundi la Gumino Wanyamulenge dhidi ya Mai-Mai. Vita hivyo vilitokea katika sehemu za Mikalati kwenye milima milefu ya Minembwe, Kivu ya Kusini.

Habari kutoka sehemu hizo zinasema kwamba mapigano yanaendelea kati ya Wanyamulenge Gumino na Wamai- mai wa kabila la Kifurero.

Mapigano haya yameacha watu wanne wakijeruhiwa kama inavyoarifiwa na mfalme wa sehemu za Basimukindji mfalme Kisale Bitorwa. Amearifu zaidi kuwa raia wa Mikalati walihamia sehemu za Mikenge kwenye teritwari ya Mwenga.

Habari kutoka sehemu hiyo zinaarifu zaidi kuwa kuna nyumba mojawapo zilizochomwa na wapiganaji.

Rediyo Okapi imetangaza ,jumatatu hii, kuwa Jeshi la Kongo limetua Minembwe kufuatilia hali ya mambo na kuleta hali ya utulivu, Makamu Kamanda wa regiment ya 3407, Kanali Bizuru amehakikisha kwamba kuna wanajeshi waliopelekwa sehemu hizo kwa ajili ya kutawanya wapiganaji hao.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Ingawa inasemekana kuwa vikosi vya walinda usalama vimekwisha pelekwa sehemu hizo, hakuna kiongozi wa ngazi za juu hata mmoja aliefika sehemu hizo wala kutoa tangazo juu ya vita hivyo.

Na tena, hakuna chombo cha habari kilichoarifu juu ya mapigano haya na hata rediyo Okapi imetangaza baada ya siku mbili za mapigano, kitendo ambacho kimechuliwa kama cha usaliti.

Raia mmoja alie karibu na sehemu hizo ameambia bwiza.com kuwa kundi la wamai mai ndilo lililoanza mashambulizi dhidi ya Wanyamulenge Gumino ambalo jukumu lake ni kuwalinda wananchi.

Raia huyu alisema kuwa chanzo cha mapigano haya ni maslahi ya baadhi ya wanasiasa wanaotaka kuwapiganisha wananchi. Huyu anasema wamekua wakishinda siku nyingi wakiishi kwa usalama, lakini siku hizi kumezuka malalamiko ya baadhi ya wananchi ya kwamba wanyamulenge wanapaswa kurudishwa kwao nchini Rwanda.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.