Taarifa kutoka mashariki mwa  nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zinasema kwamba kuna  kundi la wanamgambo la Wanyarwanda, Warundi na Waganda katika maeneo ya  Beni na Ituri.

Wabunge nchini humo tarehe 16 Octoba 2018 walisema kuna ishara za kutosha kwamba hili kundi linajiunda na kuwa watawasilisha hili suala  kwa Rais Joseph Kabila Kabange.

Kwa mujibu wa taarifa za RFI, hawa wabunge waliokuwa katika ziara ya kikazi eneo la Beni walitangazia vyombo vya habari kuwa kuna kundi la wanamgambo ambao wanafanya maandalizi yao karibu na mpaka wa mkoa wa Ituri na Beni.

Mmoja wao, Raymond Tcheda Patayi alisema matokeo ya upelelezi wa msingi yatatumwa kwa wale ambao wanahusika kwa kukabiliana na hili suala.

Ikumbukwe kwamba wanajeshi wa DR Congo ndio waliotangaza kwa mala ya kwanza uwepo wa hawa wanamgambo ambao jina lake halijatambulika kama ilivyotangazwa na Msemaji wa FARDC katika Ituri, Luteni Jules Ngongo.

Hata hivyo, kunadaiwa kwamba kundi hili linaundwa na Wanyarwanda, Warundi na Waganda wanaojiunga na  wanajeshi wa Congo kwa jina la Hindus.

Siku zilizopita kulikuwepo makundi mengine ya kijeshi kama vile MRC (mouvement pour la résurrection du Congo) kwa uongozi wa  Gen Kakolele na Kambasu Ngeve, kutoka RCD/KML ambaye alijiunga na wanamgambo wa  M23.

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.