kwamamaza 7

RCS yafunguka kuhusu kutoroka kwa Mtangazaji  Cassien Ntamuhanga

0

Baada ya mfungwa Cassien Ntamuhanga kusikika akijigamba kutoroka gereza ya Mpanga, wilayani Nyanza kusini mwa nchi.Msemaji wa ofisi kuu ya magereza nchini(RCS), CIP Hillary Sengabo amefunguka kuhusu tukio hili.

Kupita mazungumzo na Sauti ya Marekani  asubuhi hii,CIP Hillary Sengabo ameeleza kwamba suala la Cassien Ntamuhanga linawahusu polisi ya nchi.

“Mtu anapotoroka gereza,mambo yake yanahusu polisi ya nchi”CIP Hillary Sengabo amefunguka

Taarifa hizi zinasema kuwa Sauti ya Marekani imejaribu  kuuliza polisi ya Rwanda hususani  kumpigia simu msemaji wake,CP Theos Badege ili kumuuliza kama kulitolewa hati za kumkamata Cassien Ntamuhanga ila hakuitika.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pengine Sauti ya Marekani imeongeza kuwa itaendelea kujaribu hili kwa kuwa habari hii imegeuka mada kubwa.

Cassien Ntamuhanga alikamatwa mwaka 2014 na kuhukumiwa na mahakama kuu kufungwa jela miaka 25 tarehe 27 Februari 2015 juu ya uhalifu wa kuwa kitisho kwa usalama wanchi na kuhusudia maovu kwa serikali ya Rwanda.

Ntamuhanga alikuwa kiongozi wa  Radiyo Amazing Grace,alitoroka gereza 31 Novemba 2017.

Pamoja na haya,Sauti ya Marekani imekuwa ikikosolewa na watu mbalimbali nchini Rwanda hasa kupitia mtandao wa Twitter wakiilaumu kumpa fursa ya kutoa maoni mtu aliyetoroka gereza.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.