kwamamaza 7

Rayon sports kukabidhiwa ubingwa baada ya mechi yao na AZAM FC

0

Timu ya Azam FC ya Tanzania ambayo ni ya wamilki wa Kampuni ya Azam inatarajiwa hapa mjini Kigali ambako itajipima nguvu na timu ya Rayon Sports ambayo ni mabangwa wa ARPL (Azam Rwanda Premier League)

Timu ya azamu ambayo imefika uwanja wa ndenge wa Kigali Alhamisi ya tarehe 06 itacheza na Rayon Sport Jumamosi ya tarehe 8 na ndipo watakabidhiwa ubingwa walioushinda kabla ya msimu kumalizika.

Mchezo huu utapigwa Uwanja wa Nyamirambo saa tisa na nusu kwa saa za nyumbani na baadaye Rayons Sports itawaonyesha mashabiki wao majina mapya watakoichezea msimu wa michezo ujao.

Ada ya kuitizama mechi hiyo ni elfu kumi za Rwanda 10,000 frw  kwenye VIP na 3000 pande zake huku nafasi za kawaida zikilipiwa 2000 frws.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Rayon Sport ilishinda mapema kombe hili na kukataliwa  na Shirikisho la Soka la Rwanda FERWAFA kukabidhiwa kombe hilo kwa mechi yao na mahasimu wao APR FC. Na kwa hivyo wakaamua kuandaa mechi ya Kirafiki na Azam FC.

Timu hii ya Rayon Sport ndio itakayowakilisha nchi katika mashindano ya klabu bingwa Afrika na APR ambao mwishowe waliweza kushinda kombe la “Peace Cup” ,baada ya kuilaza Espoir ya Rusizi 1-0 na wataweza kucheza katika kombe la shirikisho la Afrika hapo mwaka ujao.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.