kwamamaza 7

Rais wa Rwanda Kagame ataizuru Msumbiji

0

Rais wa Rwanda mheshimiwa Paul Kagame anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi katika nchi ya msumbiji. Inasemekana kwamba katika ziara hio atatoa somo kuhusu mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya nchi ya Rwanda, mnamo tarehe ya 25 Oktoba 2016.

Taarifa ya tuvuti la Club of Mozambique, kutoka Msumbiji inasema kwamba somo hilo litafanyikiwa katika kituo cha mkutano cha Joaquim Chissano International.

Rwanda imepiga hatua kimaendeleo na kuwa na uendelevu wa uchumi kulingana na kilimo, kazi za viwandani, nkd. The Economic Magazine yathibitisha uendelevu wa kimaendeleo wa Rwanda.

[ad id=”72″]

Club of Mozambique iliandika kwamba somo hilo litakuwa wazi kwa wafanyabiashara, wasomi, watangazaji na wanafunzi.

Nchi ya Rwanda imechukuliwa bora duniani pamoja barani Afrika kwa kuwa na mazingira yanayopatana na ufanyaji wa biashara. Imechukuwa nafasi ya 62 katika nchi 189 katika Cheo cha Doing Business duniani.

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.