kwamamaza 7

Rais wa Misri yahuzunishwa na mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi

0

Baada ya kutua nchini Rwanda kwa ziara yake ya kidplomasi,Rais wa Misiri Abdel Fattah El Sisi ametembelea nyumba ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994 ya Gisozi,mjini Kigali na kuwapa heshima waliozikwa pale.Rais  Sisi amesema kwamba ana huzuni kwa ajili ya yaliyotokea na kuomba kwamba haya kutotokea mahali pengine duniani nzima.

Rais Sisi akikaribishwa na waziri wa utamaduni na michezo,Julienne Uwacu

Katika Ziara yake ya siku mbili  ilyoanza tarehe 15 mwezi wa Agosti 2017nchini Rwanda,Rais Sisi baada ya kumkaribisha kwenye uwanja wa ndege Kanombe amekwenda kuwapa heshima waliouawa katika mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994 ambapo watu miliyoni moja walipoteza maisha yao katika siku 100 tu.

Kwa kutumia lugha ya kiarabu Fattah na kuandika katika  kitabu cha wageni, Sisi ameeleza kwamba amehuzunishwa na yaliyotokea na kusema”Leo tunasikitika sana,tunakumbuka wathirika wa mauaji ya kimbali.Tunasisitiza kwamba maisha ya binadamu hayastahili kukiukiwa”.

 

Rais Sisi amendelea na kusema  kwamba anaamini kuwa vitendo vya ukatili vilivyotokea katika mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi havitatokea tena na kusema”Tunaamini kwamba vitendo vya ukatili havitatokea tena,na amani kuenea kwenye pande zote za dunia”.

Sisi ameomba watu wote kuheshimiana na kuishi kwa amani,umoja na ushirikiano pia na uhuru duniani.Rais Sisi amesema kuwa yaliyotekea nchini Rwanda ni funzo la kuwa watu kutoelewana si lazima kupambana kwa kuwa thamani ya binadamu hapa duniani ni kukaa na kuzungumza kuhusu mambo tofauti kwa lengo la kujenga ushirikiano.

Nyumba ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi ya Gisozi mjini Kigali palizikwa wathiriwa 250,000 waliouawa kutoka sehemu mbalimbali za mji Kigali.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.