kwamamaza 7

Rais wa misri kutua Rwanda kwenye ziara ya Kidiplomasi

0

Rais wa Misri Bw abdel Fattah al-Sisi atakuwa Rwanda kwenye ziara yake ya siku mbili yenye lengo la kudumisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi ya Rwanda na Misri.

Rais wa misri ambaye anapanga kufanya ziara yake kuanzia tarehe 15 Agosti ataendelea kwenye nchi kama Tchad, Gabon na Tanzania kama alivyoarifu Balozi wa Misri nchi Rwanda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mbali na kuwa ziara hii inalenga kuimarisha uhusiano ulioko kati ya Rwanda na Misri, itakuwa pia kielelezo cha nia ya serikali ya Misri ya uhusiano na ushirikiano wa kidiplomasia ulioko kati ya Misri na mataifa ya Afrika. Itakuwa pia kielelezo cha mchango wa taifa la Misri katika kutafutia suluhu matatizo yanayolikumba bara la Afrika.

Nchi ya Rwanda na Misri zimekuwa na uhusiano mzuri wa tangu siku za mbele kwa kuwa nchi hizo zina hata balozi wakilishi kwa kila nchi.

Nchi hizi pia zimekuwa zikishirikiana kwa Nyanja mbalimbali hususani kupitia makubaliano ya ushirikiano yaliyopigiwa sahihi yaani ushirikiano kiuchumi, kiufundi wa mitambo, maendeleo ya biashara na viwanda, kilimo, elimu, vijana na afya.

Ushiriakano wa Rwanda na Misri yaukwamii hapo kwa kuwa nchi hizi mbili zinashrikiana hata kwenye sekta ya miundombinu ambapo kampuni kutoka Misri itajenga kiwanda cha kusafisha maji yatakayochangia kumaliza swala la ukosefu maji kwenye maeneo mbalimbali nchini Rwanda.

Uhusiano na ushirikiano wao pia haujakwamia hapo kwa kuwa napo katika sekta ya elimu kutajengwa idara ya utafiti wa madini itakayosimamiwa na Chuo cha Cairo.

Na hapo kwenye Afya madaktari watalaam kutoka Misri wanakuja nchini Rwanda kutoa matibabu maalum kama ya kansa kwa wagonjwa ambayo yangewaghalimu sana hususani wakitaka kwanda kutibiwa nchi za ng’ambo.

Rais wa Misri anaizuru Rwanda ikifuatia ya ile ya  wakati Rais wa Rwanda Paul Kagame aliposhiriki mkutano kuhusu amaendeleo na Uchumi ambapo marais hao walikuwa na mazungumzo ya moja kwa moja.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.