kwamamaza 7

Rais wa Guinea, Alpha Conde ndie mteule kiongozi mpya wa AU

0

Rais wa Guinea Conakry ndiye amechukua nafasi ya Idriss Deby Itno wa Tchad kuwa kiongozi wa jamii ya Umoja wa Afrika, AU, kwenye sherehe ambayo ilifanyika kwenye kikao Addis Ababa nchi Ethiopia leo tarehe 30 Januari 2017.

Idriss Deby ambaye ameongoza AU mwaka moja, alikua alichukua nafasi ya Robert Mugabe wa Zimbabwe. Kiongozi mteule huongoza mwaka moja, na wanao ongoza ni marais ambao huunda jamii ya umoja wa Afrika kutoka  Kasikazini, Mangharibi, Afrika ya Kati, na Mashariki.

Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini ndiye aliongoza kwa mwanzo AU mwaka wa 2001, mwaka wa 2007 Omar Bashir alikataliwa kuongoza kwa sababu ya vita ya Darfur na aliye ongoza ni John Kufuor wa Ghana.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mwaka wa 2010 Muammar Gaddafi aliyeongoza Libya, alipenda kuongoza miaka miwili ili apate jinsi ya kujenga mpango wa nchi zenye kua katika umoja wa Afrika, ila haikuwezekana na Lybia ilikua nchi ambao ilitoa msaada wa umoja wa Afrika.

Rais kiongozi wa AU anahusika na mikutano miwili mwakani, na kusimamiya bara katika mikutano ya nchi kubwa nane ama ishirini ulimwenguni, G8 na G20.

Katika mkutano wa mwaka huu, watatangaza atakaye chukua nafasi ya Nkosazana Dlamini Zuma kwa uongozi wa Tume la AU, na atatoka kati ya Agapito Mba Mokuy wa Equatorial Guinea, Amina Mohamed wa Kenya, Moussa Faki Mahamat waTchad, Abdoulaye Bathily wa Senegal na Pelonomi Venson-Moitoi wa Botswana.

[xyz-ihs snippet=”google”]

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.