kwamamaza 7

Rais Obama awasihi raia wa Marekani kuhusu Donald Trump

0

Jumatatu hii Novemba 14 Barack Obama amefanya mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu kufanyika kwa uchaguzi wa urais ambapo Donald Trump aliibuka mshindi. Rais Obama ambaye anayemaliza muda wake amewataka Wamarekani kukubali matokeo ya uchaguzi, bila hata hivyo kumpinga mrithi wake.

Mkutano huu na waandishi wa habari ulionekana kama ni katika hatua ya kwanza ya kuaga, ambamo Obama anaendelea kushilikilia madaraka hadi Januari 20.

“Raia wameamua, Donald Trump atakuwa rais atakaye nirithi, rais wa 45 wa Marekani, alisema rais wa Marekani ambaye alifanya kampeni dhidi ya Donald Trump.

[ad id=”72”]

Na wale ambao hawakumpigia kura wanapaswa kutambua kuwa hivyo ndivyo demokrasia ilivyo, ni mfumo wetu. Nadhani ni muhimu kumuacha achukuwe maamuzi, na raia wa Marekani wataona, kwa kipindi cha miaka miwili ijayo kama wanapenda kile wanachoona, kama ni aina ya sera na mwelekeo kwa ajili ya nchi ambavyo walikua wanatarajia.

Aliendelea kusema, Nilimwambia na nayarejelea hadharani, kwamba kwa sababu ya mazingira ya kampeni hii, hasira, maneneo ya chuki, ni muhimu sana kwake kuonyesha ishara ya umoja kwa kufikia watu wachache ambao wamehisi kulengwa na hotuba alizokua akitoa wakati wa kampeni, “ amesema Rais Barack Obama.

[ad id=”72″]

Rais Barack Obama amewahakikishia washirika wa Marekani kwamba Donald Trump ataendeleza heshima na ushirikiano wa kimataifa baina ya nchi yake nao wakati yeye atakapokabidhi urais mwezi Januari.

Obama amesema kwamba Marekani lazima iendelee kuwa nguzo ya nguvu na ya matumaini kwa watu duniani kote. Na kuongeza kusema kwamba uhusiano baina ya nchi na nchi unakwenda mbali zaidi ya nafasi ya urais na wanadiplomasia,majeshi na kwamba wakuu wenye hekima na busara wataendelea kuonesha ushirikiano na wenzao wanaoshughulikia masuala ya kigeni.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.