kwamamaza 7

Rais Nkurunziza wa Burundi hatatoka madarakani

0

Katika mkutano ulipatikania Gitega tarehe 11 Oktoba 2012 nchini Burundi wa viongozi wa vyama vya siasa, viongozi walikubaliana kwamba rais Pierre Nkurunziza atakuwa mgombea urais hadi atakapochoka.

Taarifa ya habari ya redio ya kimataifa ya Ufaransa, RFI inasema kwamba mkutano huu uliongozwa na waziri wa usalama ndani; ijapokuwa maamuzi yalibaki siri. RFI inasema kwamba maamzi ya siri alitobolewa na kimoja miongoni mwa vyombo vya habari vya serikali.

[ad id=”72″]

Chombo cha habari ambacho hakutajwa kilitangaza kwamba wanasiasa wanaokubaliwa na serikali wote walikubaliana na rais Pierre Nkurunziza kuwa atagombea madaraka milele na milele.

Mmoja mwa washirika wa mkutano huu alisema kwamba katika vyama vya siasa 22, kuna ambavyo husemekana kuwa kwa upande wa wapinzani kwa kudanganya; kumbe hufanyia chini ya ushawishi wa chama cha madarakani yaani CNDD-FDD.

[ad id=”72″]

Inasemekana kwamba mkutano huo uliamua-kwa makubaliano ya CNDD-FDD- kubadilisha katiba na kumpatia rais Nkurunziza uhuru wa kugombea uongozi.

Wapinzani wa serikali ya Nkurunziza hawakubaliani na jitihada zake za kuendelea madarakani milele. Agathon Rwasa, kiongozi makamu wa bunge husema kwamba atapambana dhidi ya tendo hili la kuipatia nchi ya Burundi Pierre Nkurunziza milele na milele.

@Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.