kwamamaza 7

Rais Nkurunziza aichana ripoti ya Benjamini Mkapa, kisa Rwanda

0

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ameikosoa ripoti ya Rais mstafu wa Tanzaniya, Benjamin Mkapa  ambaye ni mpatanishi katika mazungumzo ya Warundi kwa kusema ripoti yake haikuzungumza kuhusu vitendo vya Rwanda vya kuharibu usalama wake tangu mwaka 2015.

Rais Nkurunziza ameandika hii ripoti  ya Mkapa haikuzungumza kuhusu masuala muhimu kuhusu Burundi.

Mkapa anasema kwamba alizichambua changamoto za  Burundi tangu  mwezi Aprili 2015 lakini  maandamano, kuipindua serikali kutoka Rwanda mwezi Meyi 2015, mashambulizi  (Januari 2015) na Julai 2015 na visa vya ugaidi karibu na Bujumbura hakuyazungumzia (…).” Nkurunziza ameandika katika barua.

Ripoti ya Mkapa ilishindwa kuonyesha waziwazi  mchango wa hawa watu maalumu katika masuala ya Burundi katika mazungumzo na kwa kura mwaka 2015 pia na matatizo mengine Burundi iliyokabiliana nayo.” Barua inaongeza.

Rais Nkurunziza ametia msisitizo kwamba hili jambo la kuficha ukweli ni kupoteza muda na ni kufanya siasa kama ya mbuni anavyoficha kicwa shimoni akisahau kwamba vipande vyake vingine vingali nje kwa macho ya kila mpita njia.

Siku chache zilizopita, Mkapa alifikisha ripoti kutoka mazungumzo kati ya Warundi kwa Rais Museveni. Baadaye, Museveni alitangaza Burundi inahitaji katiba nyingine.

Kwa upande wa Rwanda, viongozi nchini humo walikanusha mashtaka ya kushiriki katika kitendo cha kulenga kuipindua serikali ya  Nkurunziza kwa kusema hawana faida yoyote kupitia hili jambo.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.