kwamamaza 7

Rais Nkurunziza afunguka sababu ya kutohudhuria mkutano nchini Rwanda

0

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amemuandikia barua  Mkurugenzi wa Tume ya Umoja wa Afrika,Moussa Faki Mahamat akijulisha kuwa hatahudhuria mkutano wa kiuchumi mjini Kigali,Rwanda.

Rais Nkurunziza ametaja kwamba hawezi kuhudhuria mkutano nchini Rwanda kutokana na kuwa haamini ulinzi na usalama wake kwa kuwa Rwanda iliwakaribisha waliojaribu kuipindua serikali ya Burundi tarehe 13 Meyi 2015.

Pia Nkurunziza ameeleza Rwanda ilifanya kinyume na sheria mkataba wa kimataifa na kutoa mazoezi ya kijeshi wakimbzi asili ya Burundi wakiwemo hata watoto bila Umoja wa Mataifa (YUNA) kujadili lolote.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pengine barua hii imefafanua kuwa Rwanda iliharibu mkataba wa Umoja wa Afrika(UA) wa mwaka 1969 kwamba   wakimbizi hawaruhusiwi kufanyia maandalizi ya kuishambulia nchi yao kwa msaada wa nchi shiriki ya UA.

Hatimaye Rais Nkrunziza amesema kwamba Burundi ilishtaki Rwanda kwenye YUNA, CEPGL na SADEC hata kama suala hili halijadiliwi vilivyo.

Rais Nkurunziza amemaliza barua iliyoifikia Sauti ya Marekani,VOA kwamba kuna imaani suala hili litatatuliwa mwaka 2018.

Isisahaulike kwamba viongozi wa Rwanda walipiga marufuku madai ya kuwaunga mkono wakimbizi asili ya Burundi kuipindua serikali.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Huyu Rais ametangaza hili baada marais wa Uganda,Yoweli Museveni na Nigeria,Mohamadou Buhari kutangaza hawatahudhuria mkutano huu wa kiuchumu.

Inatarajiwa kuwa kwenye mkutano huu,marais watatia saini makubaliano ya kuanzisha soko moja la kiujumi barani Afrika.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.