kwamamaza 7

Rais Museveni kuongoza nchi hadi mwaka 2031

0

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameidhinisha mswada unaoondoa kikomo cha umri kwa wagombea urais nchini, hatua aambayo itamuwezesha kuwania tena urais mwaka 2021.

Mswada huo pia unarejesha takwa la rais kuongoza kwa mihula miwili pekee ya miaka mitano.

Kwa kuwa sheria hiyo itaanza kutekelezwa sasa, Bw Museveni anaweza akaongoza Uganda hadi 2031.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la Uganda, katibu wa rais Bi Linda Nabusayi amesema Bw Museveni alitia saini mswada huo kuwa sheria Desemba 27 na kisha akatuma waraka tarehe 29 Desemba.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Sheria ya awali ilikuwa inamzuia mgombea kuwania urais baada ya kutimiza umri wa miaka 75.

Bw Museveni kwa sasa ana miaka 73.

Hatua ya rais huyo kuidhinisha mswada huo imetoa wakati ambao amekuwa akihimizwa na viongozi wa kidini na wanaharakati wa kisiasa kutoidhinisha.

Bunge liliidhinisha mswada huu mnamo tarehe 10 Desemba kwa zaidi ya theluthi mbili ya wabunge waliohudhuria kikao, wabunge 317 wakiunga mkono na 97 wakapinga.

Asili:BBC

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.